Mtu anapolala huwa anageuka geuka, kitendo hiki ni muhimu kwa ajili ya afya.Kama mgonjwa hawezi kugeuka geuka anatakiwa ageuzwe upande kila baada ya muda.
Utafiti uliofanywa marekani umeonesha kuwa watu ambao hawana dini au imani ya mungu wapo hatarini kwa asilimia 60% kupata magonjwa ya moyo kuliko ambao wana imani.
Pia wataalamu hawa wa Saikolojia wakaongeza kuwa watu wasio na dini maisha yao ni mafupi sana kuliko wenye dini. Halikadhalika watu hawa wanasumbuliwa na maradhi mara kwa mara.
Pia tafiti nyingine zimeonesha kuwa watu ambao wanasamehe au wana uwezo wakusamehe wanakuwa na afya njema ya mwili na akili kuliko ambao hawasamehe auhawana uwezo wa kusamehe. Hivyo ni vyema kujifunza kusamehe.