Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

6- TAI anapotaka kufanya mapenzi, Jike ukimbia kwa speed kali akielekea chini kisha ananyakua tawi la mti na kupanda nalo kwa kasi angani Huku dume likimfuata kwa nyuma, kisha analiachia chini Dume anaanza kulikimbilia kabla halijatua na kulikamata KISHA kulirudisha Tena kwa Jike na Jike nae analiachia Tena mchezo wao unakuwa ni uleule hadi Jike lichoke, Jike likichoka ndo linampa mzigo dume ausasambue, Jike la TAI Huwa halitoi mzigo kwa dume lilokuwa LEGELEGE. (HII INAITWA ASIYEFANYA KAZI NA ASILE).
 
7- TAI ni Ndege ambaye yupo tofauti kabisa na walivyo viumbe wengine, kwenye swala la Hari ya hewa, viumbe wengi wa mwituni wanapata Wakati mgumu mno inaponyesha mvua kubwa yenye upepo mkali, lakini cha kushangaza TAI yupo tofauti kabisa na viumbe Hao, Yeye ujisikia raha Sana inaponyesha mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali maana ule upepo umuwezesha kuruka kwa wepesi kwenda mbali zaidi angani hadi kufika kwenye mawingu mazito kuliko kiumbe chochote kile hata hivyo bado haridhiki Anatamani kufika juu zaidi na zaidi.
 
10- Anapofika Kati ya miaka 55 Baadhi ya Manyoya yake unyofoka na kupata Wakati mgumu Sana kupaa, hali Ile usababisha kurudi ardhini na kutafuta sehem yenye pango ambapo Kuna usalama wa kutosha na kuanza kujitoa manyoya yote, na kusalia umo pangoni akila udongo na vijidudu vitakavyojipendekeza, hadi manyoya yake yatakapoota Tena upya, na kutoka mule pangoni na kupaa Tena angani kama zamani.
 
Jambo la pili

Tai wanauwezo wa kuona mbali sana. Wanaweza kuona kitu kilichoko umbali wa kilometa tano.

Tai akiona mawindo yake huangalia pale pale na huanza kwenda kukamata mawindo hayo kwa kasi kubwa. Haijalishi kama kuna vipingamizi vyovyote njiani, tai hatabadili kuangalia mawindo yake hadi akamate mawindo.
 
Tunajifunza nini?

Unatakiwa kuwa na maono na uyatazame maono yako bila kuangalia pembeni mpaka uyapate au uyatimize hiyo ndiyo siri ya kuelekea mafanikio yako, haijalishi vikwazo unavyokumbana navyo njiani, wewe kaza mwendo bila kurudi nyuma.
 
Tunajifunza nini?

Kuwa makini na kile unacholisha macho yako, masikio yako hasa kuangalia filamu na luninga. Usipende kutumia mizoga (mambo machafu) kwa sababu utaiharibu nafsi yako na maisha yako hayatakwenda kwa kasi kubwa ya mafanikio.
 
Jambo la nne
Tai wanapenda mvua kubwa na yenye upepo.
Mawingu yakikusanyika tai wanafurahi. Tai hutumia upepo wa mvua kupaa juu sana angani hata juu ya mawingu. Akifika huko juu sana hatumii nguvu nyingi kupaa anaweza kutandaza tu mabawa yake halafu anaanza kuelea bila shida akifurahia maisha mazuri.
Huku ndege wengine wakati wa mvua kubwa yenye upepo, hujificha kwenye mapango na kwenye vichaka.
 
Tunajifunza nini? Tunaweza kutumia mvua kubwa yenye upepo (changamoto) kujinyanyua juu sana . watu wote waliofanikiwa wengi wao hufanikiwa wakati wa changamoto kubwa. Wao hutumia mvua ya upepo kupaa juu sana angani tena wakati mwingine juu ya mawingu.
 
Jambo la tano
Tai hupima kwanza kabla ya kuamini.
Tai jike akikutana na tai dume na wakataka kujamiiana, tai jike hupaa kwa kasi kubwa kwenda chini wakati huo tai dume anafuatia kwa nyuma. Akifika chini huchukua tawi la mti kisha hupaa tena angani na tawi hilo huku tai dume anafuata kwa nyuma.
 
Akifika umbali mrefu angani tai jike huliachia hilo tawi na tai dume hulikimbilia mpaka alikamate kabla halijadondoka chini na akisha likamata analirudisha tena juu kwa tai jike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…