Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hurudia na kurudia mpaka kiota kinakuwa kikubwa. Kisha baada ya kuweka miiba na vimatawi vidogo vidogo vya miti, tai huyu anaenda tena chini kuchukua majani laini, akimaliza kuweka majani laini anarudi tena kuchukua miiba anakuja anaiweka juu ya kiota ili kuzuia maadui, na mwisho akimaliza hayo yote ana nyonyoa baadhi ya manyoya yake ili kuweka sehemu ya mayai yatakapokuwa iwe laini.
 
Miiba ( changamoto) ndizo zinazokukomaza kwenye safari yako ya kufanikiwa. Usizilaumu changamoto bali tafuta namna ya kukabiliana nazo huku ukijifunza kitu kutokana na changamoto hizo
 
Hata ukiwa na watoto wako, wakati mwingine wapitishe kwa makusudi kwenye mazingira magumu ili wajifunze kitu. Wapitishe mara kwa mara kisha unapomaliza kuwapitisha waulize wamejifunza nini?. Utakuwa unawasaidia.
 
Akiona hivyo huenda kwenye pango mbali na maadui, akifika humo kwenye pango hujinyonyoa manyoya yote hadi anabaki uchi kabisa. Anaendelea kujificha humo mpaka anaota manyoya mengine ndipo anatoka nje.
 
Tunajifunza nini? Wakati mwingine tunatakiwa kuziacha baadhi ya tabia mbaya ambazo zinatukwamisha kufikia mafanikio yetu makubwa.
Tabia zinazotukwamisha kupaa kwa kasi kubwa ni mzigo kwetu
 
Tunatakiwa kuziacha mara moja. Sio tabia tu bali hata maarifa. Huenda bado unaishi kwa kutumia maarifa ya zamani ambayo yanakukwamisha kupaa kwa kasi kubwa kwenye mafanikio yako, basi unatakiwa kujifunza maarifa mapya ili uweze kufanikiwa kwa kasi kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…