Magawa ni jina la Panya mkubwa wa kiume ambae anatoka Tanzania lakini anafanya kazi nchini Cambodia, Ametunukiwa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini. Magawa amenusa mabomu 39 na silaha 28 ambazo hazijalipuka katika maisha yake, Katika wanyama 30 waliowahi kupewa tuzo hiyo, Hii imekua ya kwanza kwa Panya.