Bernard alikuwa ni mpishi mashuhuri nchini ufaransa na mwenye talanta kubwa ya upishi ambaye mwanzoni mwa miaka ya 2000 alianzisha mgahawa wa Auguste Gusteau, ambao haraka ukapewa hadhi ya nyota tano.
Kauli mbiu yake ya kibinafsi ilikuwa ni kwamba mtu yeyote anaweza kupika, alikuwa mpishi mdogo katika historia katika nchi hiyo kupata mgahawa wenye nyota 5, na alikuwa miongoni mwa wapishi bora zaidi ulimwenguni.
Mgahawa huo ulipoteza moja kati ya nyota zake tano na kushushwa hadi nyota tatu baada ya mwaka 2003 mkosoaji mkuu wa chakula wa Ufaransa Anton Ego kuandika mambo machafu juu ya mgahawa huo akisema kuwa anafahamu siri zote kwakuwa yeye pia aliwahi kufanya kazi ya upishi hapo.
Bernard alivunjika moyo kutokana na mgahawa wake kushushwa hadhi, baadaye akakutwa amejiuwa. Baadaye mgahawa huu ulibadilishwa na sasa unaitwa La Ratatouille.