Mojawapo ya faida ambayo ni muhimu ni kusaidia kumeng’enya sukari mwili au kuweka sawa mfumo wa sukari mwilini na pia tatizo la kukosa choo ni tatizo la kawaida kwa wagonjwa wa Kisukari.
Tukiachana na kisukari, bamia huongeza na huboresha kinga ya mwili hasa kwa watu ambao kinga yao ya mwili imeshuka kama vile watu wenye maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).
Watu wenye matatizo ya vidonda vya tumbo, bamia huwasaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo na huongeza kiwango cha damu mwilini. Wengine wanatumia bamia kama dawa ya kuongeza kinga ya mwili kwa kutafuna zikiwa mbichi au kuzichemsha.
Ulaji wa bamia husaidia kutibu tatizo la upungufu wa damu. Bamia pia huondoa sumu mwilini na faida nyingine ni kuimarisha mifupa pamoja na mfumo wa uonaji kwa sababu ina chanzo kizuri cha vitamini A na Beta Carotene.
Bamia pia husaidia mwili kukabiliana na baadhi ya saratani. Utelezi wake huchuja uchafu unaoingia katika Kolestorali (cholesterol) na asidi ya nyongo inayoingia kutoka kwenye ini ambao usipodhibitiwa huenda ikasababisha matatizo ya kiafya.
Bamia ina Vitamin C ambayo inawafanya watoto wanaougua ugonjwa wa pumu kupumua vizuri wanapoitumia. Nusu kikombe cha bamia iliyopikwa, huwa na miligramu 13 ya vitamin C, ikiliwa husaidia sana.
Kwa wagonjwa wa kidondandugu (Cancer); wakitumia bamia husaidia kuweka utumbo kuwa na hali nzuri, hivyo kupunguza uwezakano wa kuugua ugonjwa huu wa kansa, hii hasa kwenye utumbo mkubwa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu tatizo la rushwa ya ngono katika vyuo vikuu viwili vya umma, UDSM na UDOM, Tafiti imebaini UDSM kuongoza kwa 40.5% na UDOM 38.6%.
Chanzo: JF
Saikolojia: Watu wanaosumbuliwa na Sonona (Depression) hupatwa pia na tatizo la kushindwa kutofautisha rangi kwa ufasaha, Huona kila kitu kina rangi ya kijivu.