Lakini tutahakikisha kwamba mambo yanakwenda sawa. Mke wangu pia anaendelea vizuri. Kwahiyo asanteni sana, Nawashukuru, Siwezi kusahau - asanteni."
Watoto wa rais, Ivanka na Eric, walituma tena ujumbe wa baba yao, huku wakimsifu kuwa "shujaa". Mtoto wa Trump aliongeza: "Nakupenda sana baba."
Akiwasili hospitali ya Walter Reed, rais hakupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi, lakini alikwenda moja kwa moja katika sehemu iliyotengwa ya rais, kulingana na kituo mshirika wa BBC Marekani, CBS News.