Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kunawa mikono huzuia watu wasiambukizwe minyoo wanaosababisha magonjwa. Minyoo hao ni wadogo hivi kwamba hawaonekani bila kutumia hadubini. Wao huishi katika kinyesi na mkojo, katika maji ya mito na maziwa, ardhini, na katika nyama mbichi au nyama ambazo hazijapikwa vizuri. Njia moja muhimu ya kuzuia minyoo wasiingie mwilini mwako ni kunawa mikono.
 
Pia, ukivalia viatu unapokuwa karibu na vyoo unaweza kuwazuia minyoo wasiingie mwilini mwako kupitia ngozi ya miguu. Mara nyingi watoto huweka mikono mdomoni. Kwa hiyo, ni muhimu kuwanawisha mikono mara kwa mara, hasa baada ya wao kujisaidia na kabla ya kula. Wafundishe kunawa mikono yao na kutocheza karibu na vyoo au karibu na sehemu ambazo watu hujisaidia.
 
Nawa uso kila siku
Ili kuzuia usiambukizwe magonjwa ya macho, nawa uso kwa maji na sabuni kila siku. Nyuso za watoto zinawishwe pia kila siku. Uso mchafu unavutia inzi walio na viini kwenye mwili wao. Viini hivyo vinaweza kusababisha magonjwa ya macho na hata upofu.
Yachunguze macho ya watoto wako kwa ukawaida. Macho yasiyo na ugonjwa huwa yenye unyevunyevu na yanang’aa. Ikiwa macho ya mtoto ni makavu, mekundu, yanauma, au kutoa usaha, mtoto anapaswa kuchunguzwa na mtaalamu wa afya au daktari.
 
Tumia maji safi tu
Watu hawashikwi sana na magonjwa wanapotumia maji safi ya kunywa na kuyahifadhi vizuri ili yasichafuliwe kwa viini. Ingawa inaaminika kuwa maji ya bomba ni salama na machoni yanaonekana safi, bado yanaweza kuwa na viini vya magonjwa.
 
Maji ya mabwawa, mito, matanki yasiyofunikwa au visima yana uwezekano wa kuwa na viini vingi zaidi. Kuchemsha maji huua viini vya magonjwa.
Visima vya maji vinapaswa kufunikwa. Ndoo, kamba, na vyombo vingine vinavyotumika kuchota na kuhifadhi maji vinapaswa kuoshwa kwa ukawaida na kuwekwa mahali safi, lakini visiwekwe chini.
 
Wachunge wanyama ili wasikaribie visima wala wasiingie ndani ya nyumba. Usitumie dawa za kuwaua wadudu waharibifu au kemikali karibu na maji.
Nyumbani, maji ya kunywa yawekwe katika chombo safi kilichofunikwa. Ni bora kuwa na chombo cha kuhifadhia maji chenye mfereji.
 
Zuia chakula kisichafuliwe kwa viini
Kwa kupika chakula kikaiva vizuri, unaweza kuua viini vya magonjwa. Ni muhimu nyama ya jamii za kuku na nyama nyingine zipikwe na kuiva barabara. Viini vya magonjwa huongezeka sana katika chakula chenye uvuguvugu.
 
Kwa hiyo, chakula kiliwe mara moja baada ya kupikwa. Ikiwa itakubidi kuhifadhi chakula kwa zaidi ya saa mbili, hakikisha kinahifadhiwa katika hali ya joto au kuwekwa mahali penye baridi. Kifunike chakula kilichopikwa ambacho kitaliwa baadaye. Jambo hilo litawazuia inzi na wadudu. Kipashe moto chakula hicho kabla ya kukila.
 
Usitumie chupa za kunyonyesha, isipokuwa umeziosha kwa maji ya moto kabisa kabla ya kuzitumia. Mara nyingi chupa za kunyonyesha huwa na viini vya ugonjwa wa kuharisha. Ni bora kuwanyonyesha watoto au kuwalisha kwa kutumia kikombe safi kisicho na chuchu.
 
Ondoa takataka zote za nyumbani
Inzi, mende, na panya hueneza viini vya magonjwa. Viumbe hao huzaana sana katika takataka. Ikiwa sehemu unayoishi haina huduma ya kuondoa takataka, tupa takataka katika shimo ambamo zinaweza kufukiwa au kuteketezwa kila siku. Ondoa takataka zote na maji machafu nyumbani kwako
 
Kwa hakika kuna umuhimu mkubwa wa jua kwa mimea na viumbe vingine akiwemo binadamu. Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa afya, zimebaini kuwa kuna manufaa makubwa ya kuota jua angalau kwa kiasi fulani kila siku.
 
Kwa kuwa najua unapenda afya bora, basi fahamu faida 10 za kuota jua kiafya.

Kuua bakteria
Jua linaweza kutumiwa kuua bakteria mbalimbali katika majeraha na ngozi. Tiba hii iligunduliwa na mshindi wa tuzo ya Nobel Niels Finsen. Tiba hii ilitumiwa kuponya vidonda vya wanajeshi wa Kijerumani baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…