1. Mdomo: Harakati za usagaji chakula huanzia mdomoni. Mdomo una meno, ulimi pamoja na maezi ya mate (salivary glands). Meno husaidia kuvunja vunja chakula kuwa vipande vidogo vidogo zaidi. Matezi hutoa mate ambayo husaidia katika usagaji wa chakula kiwe kilaini zaidi baada kuvunjwa vunjwa, pia hukitia unyevunyevu zaidi vyakula vya wanga kiasi kwamba kiweze kumezwa kwa urahisi zaidi. Ulimi hukichanganya chakula kwa mate na tena hukiviringisha chakula kuwa matonge madogo madogo na kuyasukumiza kwenye koo.