III. Badilisha mtindo wa maisha yako
Kutosagika chakula kunaweza kusababishwa na mfadhaiko unaotokana na shida za kimaisha, tabu dhiki, matatizo na mambo kama hayo.
Jaribu dawa.
Kama kutosagika kwako chakula hakujakuletea tatizo kubwa sana, basi jaribu dawa za kuzima asidi (anti-acid) ambazo hufanya kazi ya kubatilisha asidi ya tumbo na kuifanya isiwe na madhara.
Kupwa kwa asidi (Acid reflux)
Asidi ndani ya tumbo zinaweza kuchoma chini ya koo na kusababisha kiungulia, maradhi yatokanayo na kupwa yanaweza kuwa na sababu tofauti tofauti.
Ngiri (Hiatus hernia)
Kiasi cha mpasuko wa sehemu ya juu ya tumbo kupitia kiwambo (diaphgram) husababisha ngiri, ni kawaida sana hasa kwa watu wenye uzito mkubwa wanawake na wagonjwa wanasikia kuingulia pindi wanapolala kwa kunyooka au kujikunja.
Ugumu unaoota kwenye nyongo (gallstone)
Nyongo ni maji maji yenye mchanganyiko wa rangi ya njano na kijani (yellowish-green) yanayotengenezwa katika ini, kisha yakahifadhiwa katika kibofu nyongo (gall bladder) na kupelekwa katika mahala ambapo husaidia kuyeyusha mafuta. Wakati mwengine kutosagika kwa chakula kunaweza kusababishwa na ugumu unaoota kwenye nyongo.
Vidonda vya tumbo (ulcer)
Kidonda chenye pepsini ni baka bichi ambalo hutokea katika kunyazi za tumbo au duodeni aisha kwa sababu kuna asidi nyingi sana ama utetelezi wenye kuzui asidi ni mdogo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.