Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Nyongo kutoka katika ini huanza kufanyia kazi mafuta wakati maji ya kongosho (Pancreatic juice) kutoka kwenye kongosho husaga sehemu ya protini na wanga ambayo haukusagwa. Kuta za utumbo pia hutoa maji ambayo husaidia kukamilisha usagaji wa wanga, protini na mafuta. Chakula kilichosagwa hufyonzwa kwenye damu, na damu hukipeleka chakula hicho katika sehemu zote za mwili.