Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyongo kutoka katika ini huanza kufanyia kazi mafuta wakati maji ya kongosho (Pancreatic juice) kutoka kwenye kongosho husaga sehemu ya protini na wanga ambayo haukusagwa. Kuta za utumbo pia hutoa maji ambayo husaidia kukamilisha usagaji wa wanga, protini na mafuta. Chakula kilichosagwa hufyonzwa kwenye damu, na damu hukipeleka chakula hicho katika sehemu zote za mwili.
 
5. Utumbo mpana (Large intestine): Chakula kilichobaki amacho hakijasagwa na hakikufyozwa huingi katika utumbo mpana pole pole kwa mafungu madogo. Utumbo mpana ni mfupi zaidi ya utumbo mdogo lakini utumbo mpana hufyonzwa sehemu kubwa ya maji na kuyapeleka katika damu.
 
Chakula ambacho hakikusagwa huhifadhiwa na utumbo mpana na kuwa uchafu (faeces) na baadae hutolewa. Ufyozanji wa chakula huaanza muda mfupi tu chakula kinapoyeyuka ndani ya maji kwahio ni muhimu sana kunywa maji mengi sana kila siku.
 
Kama baada ya kula na kupata dalili yoyote miongoni mwa hizo tutaiita hali hiyo ni kutosagika kwa chakula (Indigestion). Watabibu huiita " Dyspepsia" dalili hizo hutokeza kama kuna kitu kinaleta matatizo katika koo au tumboni.
 
Chakula kinapowasili kunyazi cha tumbo huanza kuzalisha asidi ili kuvunja vunja chakula na kukifanya kiwe rahisi kusagika. Asidi ina nguvu sana na kama ingekuwa peke yake bila kuwepo tabaka la mnyunyizo uliogandana unaoitwa utelezi (Mucus) ambao huzifunika kunyazi ili kuilinda, asidi basi ingeweza kulimong'onyoa tumbo lote.
 
Sababu hasa ya kutosagika chakula tumboni ni kula sana au kunywa kupita kiasi au kula mlo usio sawa pombe vyakula vya mafuta mengi kama chipsi vyakula vyenye asidi nyingi kama vile machungwa lakini kwa bahati mbaya au nzuri hakuna seti moja ya kanuni juu ya ule nini au usile nini. Watu hutofautiana katika kudhurika na vyakula, hivyo ni suala tu la kuainisha mwenyewe ni chakula gani ambacho kinakudhuru na halafu akakiacha.
 
Namna mbalimbali za vyakula vinaweza kuuvuruga ulingano wa asidi na utetlezi. Vile vile uvutaji sigara madawa (kama vile aspirini) au matatizo ya mhemko (emetional problems) huwa ndio sababu kuu, na mara nyengine hakuna sababu ya wazi zaidi
 
Mara kwa mara tatizo la aina hii la kutosagika chakula hujimaliza wenyewe hatimaye. Utakapoacha kutumiwa dawa au kubadilisha dawa na kutumia aina nyengine za dawa za matatizo ya mihemeko yataondoka kunyanzi za tumbo nazo zitajikarabati wenyewe na tatizo la kutosagika chakula litakwisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…