Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BADALA YA KUHANGAIKA NA JAMBO LISILOWEZEKANA KAENI CHINI MJIULIZE NINI MLIKOSEA?

Niwasaidie (haswa CHADEMA) kwa kuwapa baadhi ya mambo makuu yaliyofanya mpate anguko kuu:

1. Uhaba wa fedha na vitendea kazi kipindi cha kampeni. Kaeni chini mjiulize mapato ya chama yalienda wapi hadi kila mgombea akaachwa aogelee kivyake? Iko wapi ruzuku ya milioni 350 kila mwezi? Iko wapi michango iliyotokana na kadi kwa wanachama mnaodai ni milioni 6? Yako wapi makato ya wabunge? Je marafiki wa ndani na nje michango yao ilienda wapi?

2. Ni kwa nini viongozi wa chama na mgombea uraisi hawakutangaza sera zilizoko kwenye kijitabu? Nini kilifanya wageuze Magufuli, Chato, Sabaya ndio sera za kujinadi kwenye kampeni?

3. Ni kwa nini mgombea uraisi alijinadi kuwa ana watu wa nje ndio wanamuunga mkono? Hii haikuharibu kampeni yenu? Kwa nini sasa msimuulize hao watu wa nje ni kina nani na sasa wamesaidia vipi chama chenu?

4. Ni kwa nini hoja muflisi kama ya ushoga, kulisha mifugo mbuga za wanyama, majimbo, maendeleo ya kikabila, n.k. hazikukanushwa haraka na bila kupepesa au kujiumauma? Nini kilizuia viongozi wa chama wasikanushe na kujitenga na hoja hizi? Hawajuona madhara kwa kampeni na chama?

5. Ni kwa nini uongozi wa chama uliruhusu udini kushamiri katika kampeni ya mgombea uraisi kiasi kwamba uongo kuwa wasilamu wote wamekubali kuwapa kura ukatamkwa hadharani? Hivi viongozi hawakuona madhara ya kuonyesha udini katika kampeni?

6. Ni kwa nini mgombea uraisi alijikita katika sera za kuvunja muungano? Kwa nini viongozi hawakuona hili? CHADEMA ingeumia kama ingeacha ACT ifuate sera za Sefu za kupinga muungano? CHADEMA imenufaikaje na kushabikia hoja za kina Sefu na UAMSHO?

7. Ni kwa nini mgombea uraisi aliachwa ageuze kampeni ni dhidi yake na Magufuli badala ya kampeni baina ya CHADEMA na CCM? Kwa nini aligeuza kampeni ni yake yeye na sio ya chama chake? Je hamkufanya kosa kuzua kauli mbiu kuwa NI YEYE? Hamkuona wenzenu kauli mbiu zao hazikulenga mtu bali chama? 5 tena Kazi iendelee!

7. Mwisho mjiulize kama uongozi haukuwa na maona kiasi hiki na wala haukuandaa fedha na vitendea kazi kwa ajili ya kampeni je bado unafaa kuwaongoza au sasa ni wakati wa kuleta damu changa na mpya?

8. Nini haswa ilikuwa mantiki ya kuwakataa watu mliowachagua kwenye mkutano mkuu kuwa wagombea uraisi zanzibar (CHADEMA) na mgombea uraisi JMT (ACT)? Hamkuona kuwa mlitoa picha kwamba hamko makini kwenye uteuzi? Hivi hamkuonyesha kuwa ninyi hamna demokrasia kwenye vyama vyenu bali udikteta? Mtu achaguliwe kwa kura kwenye mkutano mkuu halafu aondolewe na mtu kwa hotuba jukwaani?

Nina uhakika mkikaa na kutafakari haya na kuacha ndoto za maandamano au za wajomba toka nje kuja kuwasaidia mtaweza kutibu mgonjwa ambaye yuko ICU. Mkijidanganya kuwa mna mwamba atawavusha, sasa basiii, kuna kina Amsterdam, kuna The Hague n.k. mgonjwa atakufa jumla. Huenda 2025 CHADEMA na ACT vikawa historia au viapande vipande kama CUF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…