Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kutengenezewa muvi? Mbona hiyo siyo ishu kivile? Labda useme muvi yenye maudhui chanya. Idd Amin ana muvi na documentaries kibao. Adolf Hitler je?

Nadhani Mandela na Gandhi wanapendwa sana kimataifa sababu ya falsafa yao kuhusu matumizi ya njia za amani katika kudai haki. Japo Mandela alikubali Umkontho we Sizwe (tawi la ANC lililohalalisha matumizi ya nguvu katika kudai haki), alipotoka jela na kuukwaa uraisi aliunda tume ya maridhiano na akasisitiza sana Waafrika kutolipiza kisasi dhidi ya wazungu (akina Malema mpaka leo wanamuita msaliti - sellout). Sidhani kama angetoka jela akiwa amewaka na msimamo mkali wa kulipiza kisasi dhidi ya wazungu kwa kutaifisha mali zao au kuwaondoa katika sekta muhimu za uchumi angepata umaarufu huu wa kimataifa. Ni kwa sababu hii hii naamini pia Martin Luther king Jr leo pia ni maarufu sana duniani kote. Vinginevyo wote hawa wangeishia tu kuitwa viongozi wa vikundi vya kigaidi au historical lunatics!

Ukitaka kuwa maarufu kimataifa, wapende wazungu hata kama walikufanyia ubaya wa aina gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…