Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nb. Sio muumini wa Conspiracies hivyo siamini eti mandela alikua crone.
Hebu tujiulize hivi Kwanini muda mwingi Gandhi kaenda sana SA??? Though wameishi vipindi tofauti
Halafu imetokea kabisa wote kupendwa na wazungu...Mimi naamini CIA wakikusifu basi kuna mahali upo wrong!! Siamini kama mandela alikua anaamini katika kutumia amani kuliko Kwame,Lumumba,Nyerere, nk nk.

Naamini kwamba (mawazo yangu binafsi) kuba vitu wanafaidika wazungu ndio maana wanaasifia. Kwa india sijajua wanafaidika nini hasa ila kwa SA tunaona jinsi walivyomiliki ardhi na Maeneo yenye thamani kama wapo kwao. Ni kama hvi kenya pia wanavyowasifiwa kwasababu bado wameweza kumiliki vitu nchini humu.
Kama kigezo ni kwa kutumia Amani basi Nyerere wangemsifu maana kaweza kutuunganisha makabira 200+ (?) Au wangemsifu St Francis wa Asizi u Sidhartha Gautama nk...

Wanamsifu Gandhi wakati bado walimuachia nchi huku wameshawawashia mgogoro na Pakistan.

Nyerere kuwaunganisha nyie makabila 120+ kunawasaidia nini wao? Wanapata faida gani kwa nyinyi makabila 120+ kuungana?

Wazungu wanachojali ni interests zao tu basi. Afrika Kusini ndiyo walipata uhuru lakini njia kuu za kiuchumi zote bado zimo mikononi mwa wazungu. Na wengine watakwambia pengine hali imezidi kuwa mbaya zaidi. Mandela ndiyo watamuona ni shujaa sana kwa sababu hakugusa interests zao. Fikiria kama angekiwasha kama Mugabe akidai ardhi warudishiwe Waafrika akataifisha na mamigodi yote na kuwapa weusi. Akadai na reparations? Unafikiri wangekuwa wanamsifu? Unafikiri wanamsifu kwa vile alikaa jela miaka 27 na hatimaye kuwa rais? Come on man!

Hata Kenya wangewafurusha akina Lord Delamere, wakachukua ardhi ile na kuwagawia Waafrika unafikiri Kenya ingekuwa inaonwaje?

Gandhi alitekeleza ile falsafa "ya kuchapwa shavu la kushoto na kugeuza la kulia" na aliweka misingi ya amani dhidi ya wazungu. Ni role model wa kudai uhuru kwa njia za amani. Igeni mfano wa Gandhi na siyo lazima kupambana.

Unajua kuwa hata Saddam kuna kipindi alikuwa shujaa sana kwa wazungu? Hata Osama - the fighting prince wakati ule anawasaidia kupambana na Warusi kule Afghanistan....

Ukiona hawa jamaa wanamsifia mtu mchunguze sana. Kwa namna moja au nyingine watakuwa wanafaidika ama kiuchumi, kisiasa, kihistoria na hata kisaikolojia. Vinginevyo they don't care aisee....

[emoji1427][emoji1427][emoji1427] Mandela...

 
ideas with no photo shop.[emoji16][emoji16]
IMG_20201206_183317_509~2.jpg
 
Back
Top Bottom