Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ki ukweli ukiwa una UPENDO hautaweza kumkosea mwanadamu mwenzako, na vitendo kama vile Chuki, Hasira, Tamaa na Ubinafsi huondoka kwani badala ya mtu kujijali yeye mwenyewe kwa mapenzi ya UBINAFSI basi hataweza kuishi na wengine.
 
Upendo sio tu uliozoeleka wa Jinsia mbili tofauti, upendo tunaouzungumzia hapa ni Universal Love, Upendo juu ya Ulimwengu na vyote vilivyopo, Upendo kwa wanadamu wengine bila kujali umri, jinsia, kabila, nchi, au imani/dini.
 
Upendo juu ya mazingira, mimea, mito, milima na kila kitu. Ukiweza kuishi kwa kutazama upendo mkuu kama wa yule Aliyepelekea uwepo wa vyote hivi utaweza kuona maisha ni furaha na upendo huchochea furaha.
 
Ki ukweli ukiwa na upendo kwako wewe binafsi, upendo kwa wanadamu wengine na upendo wa kwa kila kinachokuzunguka utaishi kwa haki, na amani kabisa. Hutaweza kujidhuru wala hutaweza kumdhuru mwenzako kabisa.
 
Back
Top Bottom