Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
FB_IMG_16093367760389700.jpg
 
Dr IGNAZ SEMMELWEIS : MWENDAWAZIMU ANAYEKUMBUKWA NA DUNIA
Wote tunajua kuwa kwa sasa hivi dunia inahangaishwa na gonjwa hili la corona
Inakadiriwa ni zaidi ya watu million 20 wameathirika na ugonjwa huu huku ikikadiriwa zaid ya vifo laki 5 duniani kote
Wanasayansi walitoa mapendekezo mbali mbali kama njia ya kujikinga na kuzuia ugonjwa huu usienee kwa kasi , na mojawapo wa njia hizo ni kuvaa barakoa, kunawa mara kwa mara kwa maji tiririka huku ukitumia sanitizer, kujitenga , na kupeana nafasi
Lakin je unajua ni nani aliyeanzisha wazo hili la kunawa mikono kama njia mojawapo ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko??
Si mwengine bali ni Daktari kutoka nchi ya Hungary aliyeitwa Dr. Ignaz Semmelweis.
Akiwa na miaka 24 alikuwa anafanya kazi katika hospital kuu ya Vienna kulitokea gonjwa la mlipuko lililoitwa mafua ya puerperal ambayo yalikuwa yanawauwa zaidi wanawake waliokuwa wanajifungua
Wingi wa vifo hivyo ulipelekea madaktari wengi kujiingiza katika tafiti mbalimbali za kutafuta tiba ya ugonjwa huo ambapo mmoja wa madkari hao ni Ignaz Semmelweis
Katika tafiti zake aligundua kuwa katika wodi mbili katika hospital yao zinazohudumia wazazi zinarekodi idadi tofauti ya vifo
Wodi ya moja ya wazazi iliyokuwa inahudumiwa na madaktari wa kiume na wanafunzi wanaosoma udaktari ilikuwa inarekodi idadi ya juu zaidi ya vifo ukilinganisha na wodi inayohudumiwa na wakunga
Lakini kwenye utafiti wake pia alikuja kugundua kuwa ugonjwa huo wa mafua ya puerperal haukuwa ukiuwa wazazi pekee bali hata watu wengine nao wanakufa na ugonjwa huo
Katika tafiti zake aligundua kuwa sababu ya wanawake waliokuwa wanahudumiwa na madaktari kuwa kubwa kuliko ile inayohudumiwa na wakunga ni MADAKTARI WALIKUWA WANAFANYA KAZI YA KUWAHUDUMI WAGONJWA WENGINE huku wakunga hawakuwa wakihudumia wagonjwa wengine tofauti na wazazi
Hivyo akagundua kuwa kutokana na madaktari wanahudumia wagonjwa wengine tofauti na wazazi hivyo kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa wanapohudumia wagonjwa wengine huwenda ikawa wanabeba virusi hivyo kisha wanapokuja kuwahudumia wazazi inakuwa rahis kuwaambukiza
Alichoamua ni kuwa Madaktari wote wanaohudumia wazazi walitakiwa wanawe mikono yao kwa maji pamoja na chlorine
Madaktari walikuwa wanamlaumu na hawakukubaliana na wazo hili kwa sababu walihisi kuwa Dr. Ignaz anawatuhumu kuwa wao ndio wanawaambukiza magonjwa wazazi kwahiyo kukawa na uadui kati ya madaktari na Dr. Ignaz
Licha ya kuwa wazo Lake hilo lilifanikiwa kupunguza idadi ya vifo kwa akina mama lakini Dr Ignaz alifukuzwa kazi na baadae akapelekwa katika kituo kinachohudumia wagonjwa wa akili akihisiwa kuwa ni mgonjwa wa akili ambako alifariki huko huko
 
Pua za wanawake zina uwezo mkubwa zaidi wa utambuzi na kutofautisha pia harufu mbalimbali kwa haraka kuliko wanaume, Sababu inatajwa kuwa wanawake wana uwepo wa seli nyingi zaidi zinazosaidia utambuzi wa harufu kuzidi wanaume.
 
Back
Top Bottom