Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Faida za supu ni nyingi, kwa ufupi ni kama ifuatavyo: Supu husaidia kuamsha hamu ya kula kwa yule aliyekuwa hana na humuongezea hamu ya kula kwa yule aliyenayo.
 
Faida za supu ni nyingi, kwa ufupi ni kama ifuatavyo: Supu husaidia kuamsha hamu ya kula kwa yule aliyekuwa hana na humuongezea hamu ya kula kwa yule aliyenayo.
 
Iwapo itatokea mtu hakupendezwa na ladha au harufu ya chakula, supu humsaidia kuficha au kuisahau hadha hiyo.
 
Kwa kuwa nivigumu kujua ni chakula kipi kitamfaa yupi, ni vyema kuwa na angalau supu pembeni kama ziada ya mlo.
 
Supu hurahisisha mlo kuwa kamili hasa kwa wale wasioweze kutafuna au kula vyakula vya kawaida, mathalani, wagonjwa, wazee, vibogoyo au watoto.
 
Mfano kwa mtu mwenye meno mazima atakula nyama, atakuwa sawa na mzee au kibogoyo atakae kunywa supu yenye mchuzi wa nyama usioungwa.
 
Kwa upande mwingine mgonjwa anaweza kukataa kula aina fulani ya chakula na labda pengine ni muhimu kwa afya yake, kinachoweza kufanywa ni kutengeneza supu kutokana na chakula hicho na kuichanganya na michuzi ya vyakula kisha kumpatia mgonjwa.
 
Badala ya kununua vinywaji baridi vyenye kuburudisha lakini visivyonufaisha mwili zaidi ya kukufilisi, ni bora kujenga tabia ya kujiandalia na kunywa supu.
 
Hii hutokea hasa kwa wale wanaotunza uzito wao usiongezeke, ambapo hupunguza kula na badala yake kunywa supu na kuifanya afya kundelea kuwa nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…