Usijilinganishe na watu wengine ambao tayari wanaweza. Ni kweli kuwa muhimu kuangalia wengine waliopiga hatua zaidi yako ili kujifunza mbinu walizotumia, makosa yao na labda mambo gani wewe unaweza kuiga, hata hivyo kosa unalofanya ni kuwaangalia hao watu kwa upande mmoja tuu wa mafanikio yao na kuona "wanakutisha". Kumbuka hata wao nao walikua na muda ambapo walikuwa kama wewe , yaani wanaanza.