Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mabadiliko haya, yanahitaji mjasiriamali sio tuu ajue vema kuzalisha bidhaa yake, ila aifahamu vema jamii anayotaka kuiuzia bidhaa, ajenge mtandao mkubwa na wateja wake, na zaidi sana aweze kukusanya na kusimamia taarifa za jinsi ya kuboresha ushindani wake katika soko.
 
Utitiri wa taarifa: Maboresho katika teknolojia ya habari na mawasiliano, yamechangia sio tuu kuwepo kwa websites na mitandao ya kijamii (social networks) bali yamerahishisha matumizi na hata umiliki wa mitandao. Mfano kuna blog kibao Tanzania pekee, na kurasa maelfu za Facebook. Kuna video mamilioni kwenye Youtube.
Usipoweza kutawala vema hali hii ya utitiri huu wa taarifa unaweza kujikuta unakuwa mtu wa kupotoshwa, na mtu usiye mfanisi katika mambo yako ya kielimu, kikazi na hata kibiashara. Hakuna wakati unaohitaji ujuzi wa kipekee wa kutawala muda wako, na pia kuweza kuchambua taarifa unazozipata.
 
Maboresho makubwa katika teknolojia mbalimbali: Si tuu upande wa teknolojia ya habari, bali aina nyingi za teknolojia kama vile teknolojia za uzalishaji wa vyakula na teknolojia za utengenezaji wa mashine. Mambo haya si tuu yanaleta bidhaa mpya na kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa mambo mengi, pia yanaleta athari nyingine ambazo inatupasa kuwa makini nazo kama vile, athari za kiafya , athari za malezi (kuporomoka kwa maadili), athari za kiuchumi (biashara nyingi kuporomoka kwa kushindwa kushindana).
 
Uharaka wa usambaaji wa mabadiliko: Kwa jinsi dunia ilivyo ‘kijiji’ mabadiliko yanayoendelea makubwa ya kiuchumi, kiteknolojia, kisiasa , na kijamii yanaathiri si tuu taifa moja ambapo badiliko fulani limetokea, bali mabadiliko hayo husambaa kwa haraka kwa nchi nyingine. Kama ilivyo kwenye usambazi wa bidhaa mbalimbali unavyosambaa kwa haraka – kumbuka matoleo kadhaa ya simu kama iphone, Samsung, n.k yanavyofikia Bongo, tutarajie mabadiliko mengine yanayotokea nchi za maghariba na barani Asia kufika kwa haraka hata Tanzania.
 
Elimu ya darasani pekee haitoshi kukusaidia kupita na kutawala mabadiliko haya makubwa, unahitaji kupenda kusoma ziada.
Hakikisha unapata taarifa sahihi kwa kufuatalia kuaminika kwa chanzo cha taarifa. Pia tumia search engine kama Google, kutafuta vyanzo vingine vya habari vinasema nini kuhusu taarifa unayodhani ni sahihi.
Linda sana utashi wako kwa kuwa huo pekee ndio mali kubwa zaidi kwa maisha yako. Ukipoteza utashi wako kwa tamaa ya mali, kufuata mkumbo n.k utajikuta unapotea zaidi.
Kuwa tayari kubadilika kuendana na mazingira na hali halisi – elimu, aina ya biashara, aina ya kazi, mahali pa kuishi, mahusiano, malezi ya watoto.
Katika nyakati tulizopo, ni muhimu sana kuufahamu na kuuishi msemo huu “ Don’t Work Hard, Work Smarter”yaani “ Usifanye tuu kazi kwa nguvu zako zote, bali fanya kazi kwa akili zaidi”.
 
FB_IMG_1611809199987.jpg
 
Back
Top Bottom