Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Zipo sababu nyingi zimetajwa kuwa zinaweza kumfanya mtu aishi kwa furaha ambazo ni pamoja na kumuamini Muumba wako; Kuwa na upendo kwa ndugu na jamaa, kudumisha amani ya moyo wako, huku ikitajwa furaha hiyo kuwa ni moja ya sababu zinazoweza kukufanya uwe na afya nzuri.Leo nimekutana na hii ya njia sita ambazo furaha inaweza kuimarisha afya yako.
 
Furaha huulinda moyo wako,-Utafiti unaonesha kuwa asili ya upendo na furaha siyo moyoni lakini husaidia kuulinda huku ikibainika kuwepo kwa uhusiano baina ya furaha na vipimo vingine vya afya ya moyo kama vile muda unaotumika wakati wa pigo moja la moyo na lingine na kuzilinganisha na hatari kadhaa za magonjwa ya moyo.
 
Furaha huzuia mkazo (stress)-Mkazo (stress) hausababishi matatizo ya kisaikolojia pekee bali pia husababisha mabadiliko ya ki-biology katika homoni zetu na shinikizo la damu. Furaha inatajwa kupoza hasira za athari hizi na wakati mwingine kutusaidia kurudi katika hali ya kawaida kwa haraka.
 
Watu wenye furaha hawaumwi mara kwa mara na huwa na kiwango kidogo cha maumivu-Watu ambao wana mood nzuri wana nafasi nzuri sana ya kuimarisha furaha ambayo huwasaidia kutoumwa homa za mara kwa mara na huwa na kiwango kidogo cha maumivu tofauti na watu ambao wana mood mbaya.
 
Furaha hurefusha maisha-Watu wenye furaha huweza kuishi kwa miaka 7-10 zaidi tofauti na wasiokuwa na furaha. Katika utafiti uliofanywa kwa wazee 4,000 wa Uingereza wenye umri wa miaka 52-79 ambao walikuwa na furaha mara nyingi zaidi kwa siku na kuonesha kuwa watu wenye furaha.
 
Pengine wewe ni mmoja wa wale wenye kupenda kweli kweli kupiga hatua. Hauridhiki na hali uliyo nayo na unahitaji zaidi, hata hivyo ni kama umekata tamaa hujui uanzie wapi kwani unajiona wazi bado upo nyuma sana vitu vingi.
 
Yaani kama unahitaji kupiga hatua basi itakuchukua muda mrefu sana, na pengine kwa ugumu huo na ukubwa wa kazi ya ziada unayotakiwa kufanya unajihisi kuishiwa nguvu.
 
Nataka nikupe moyo, sio wewe peke yako wengi tumepitia huko. Hata hivyo njia rahisi ya kuondokana na hizo hisia ni kufikiria kinyume cha hizo hisia. Inawezekana kushinda hizo hisia na ukajikuta unasonga mbele na mambo yako. Jinsi ya kushinda ni kama ifuatavyo:
 
Usijilinganishe na watu wengine ambao tayari wanaweza. Ni kweli kuwa muhimu kuangalia wengine waliopiga hatua zaidi yako ili kujifunza mbinu walizotumia, makosa yao na labda mambo gani wewe unaweza kuiga, hata hivyo kosa unalofanya ni kuwaangalia hao watu kwa upande mmoja tuu wa mafanikio yao na kuona "wanakutisha". Kumbuka hata wao nao walikua na muda ambapo walikuwa kama wewe , yaani wanaanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…