Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kumbuka ulipoanza kusoma A, E mpaka Z ? Kumbuka enzi hizo hata kujumlisha hujui ? Basi maisha ndio hivyo, kuwa mambo makubwa huhitaji kujengwa kidogo kidogo. Na hakuna namna ya kufika kwenye ukubwa bila kupitia udogo. Hivyo anza kidogo kidogo. Ni kweli hautoona mafanikio mara moja, ila jua kuwa baada ya muda hivyo vidogo vidogo unavyovifanya vitajenga kitu kikubwa. Na hapo ndipo utakapofikia mbali huko unakotamani kufika.
 
Jiwekee utaratibu wa kuchambua malengo yako yaani katika kila lengo lako kuu mfano KUJUA ENGLISH VIZURI, uwe na malengo madogo basi unaweza kuwa na lengo la kujua vizuri Tenses, kujua vizuri Adverbs, kuboresha wingi wa vocabulary, n.k Kwa kadri unavyotimiza vijimalengo vidogo vidogo , ndivyo unavyokaribia lengo lako kubwa.
 
Jiwekee taratibu ya kupima mafanikio yako madogo madogo na kujipongeza. Usisubiri mpaka lile lengo kuu lifikiwe. Unajua kuwa jambo kubwa kubwa huundwa na mambo madogo madogo unayoyafanya na kufanikiwa. Jipe moyo , unaweza, na utaweza.
 
Unajiona wazi kuwa umetingwa na mambo mengi, Siku inaanza na kuisha na ukitafakari mambo gani haswa umefanya kwa ajili ya "future" yako huyaoni, zaidi ya yale uliyofanya kwa ajili ya sasa, iwe kazini, au kuenda darasani, au kuenda kwa biashara yako kufanya shughuli za kila, na sio yale mengine ambayo unajua ndio yatakayokusaidia kupiga hatua toka hapo ulipo.
 
Nataka ukumbuke kitu kimoja, daima hautokuwa na muda wa kutosha kwani ukweli sio kwamba watu wanafanya mambo makubwa kwa kuwa wana muda wa kutosha, bali ni kwakuwa wanapangilia VIPAUMBELE.
 
Hivyo angalia mambo gani uliyonayo sasa uyatoe katika vipaumbele vyako ili uingize mambo mengine unayohitaji haswa haswa yawe kama vipaumbele. Hivyo badala ya kutumia DK40 kuwa mtandaoni kusoma mambo yasiyo na msingi kwa "future" yako, tumia hizo dk40 kusoma kitabu chako cha English.
Huo ni mfano tuu wa kusoma English. Kuna mambo mengine mengi ambayo wewe unahitaji kuyafanya. Yaweke ktk kipaumbele.
 
Uhuru wa mawasiliano: Uwepo wa mitandao ya kijamii, kushuka kwa bei za simu na kompyuta , teknolojia ya upigaji picha na uandishi kama vile kutumia blogs, ni baadhi ya mambo yanayochochea uhuru wa mawasiliano kukua. Uhuru huu unaweza athiri malezi ya watoto, uhuru pia unaweza athiri usiri wa mambo yako, na bila shaka unaathiri ufanisi wako kibiashara na kikazi pia.
 
Ili kuweza kujitawala na kutawala mabadiliko haya ya uhuru wa mawasiliano, inakupasa ujifunze vema matumizi ya teknolojia husika, au upate mtu wa kukusaidia kusimamia mambo yako ili yasiathirike na uhuru huu wa mawasiliano.
 
Fahamu yapi unastahili kufanya ukiwa mtandaoni – kwa simu na kwa kompyuta, tambua pia nini watu wanafanya ambayo yanaweza kukuathiri. Mfano mzuri, ni pale unapoweka picha ya mpenzi wako aliyependeza vizuri, ila picha hiyo ukaikuta imewekwa kwenye mitandao ya ngono.
 
Mfano mwingine, usipofuatilia mara kwa mara anachoandika mtoto wako mtandaoni unaweza kushtushwa siku ukawa tagged picha binti yako aliyepo ‘boarding school’ akila ‘bata’ kwenye club ya usiku. Au kukuta ameandika status – “ Jamani, siwezi soma huyu BF wangu kila nimfanyiacho haridhiki, nimempa hadi pocket money zangu akae nazo, ila haridhiki”.
 
Machafuko katika jamii: Hali ngumu ya kiuchumi, mabadiliko katika uwezo wa kifikra wa watu, na ukandamizaji uliokithiri katika jamii zetu ni moja ya sababu zinazochochea machafuko ya kila siku yanayoendelea. Hata yale ambayo ulidhani kuwa hayawezi kutokea nchini mwetu, bila shaka utaanza kuyaona yakitokea.
 
Hali hii ni muendelezo wa mabadiliko makubwa katika maisha yetu. Serikali zinazidi ‘kuchangikiwa’ kwakuwa mabadiliko yanatokea kwa haraka sana na ni mabadiliko makubwa ambayo hayakutazamiwa. Hivyo serikali kujibu mapigo haya, inabidi zije na mbinu nyingi kali zinazoweza kuonekana kama ni za kidikteta.
 
Uzalishaji mkubwa wa ushindani wa hali ya juu: Kupanuka kwa fikra za watu wengi, maboresho katika teknolojia, urahisi wa upatikanaji wa taarifa, na mijumuiko ya watu toka mataifa tofauti katika nchi tofauti,ni mambo yanayoleta ushindani katika uzalishaji. Mbinu zilizosaidia biashara fulani kuwa kubwa miaka 10 iliyopita, zinaweza zisiisaidie biashara hiyo hiyo, au nyingine inayofanana nayo kukua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…