Elimu ya darasani pekee haitoshi kukusaidia kupita na kutawala mabadiliko haya makubwa, unahitaji kupenda kusoma ziada.
Hakikisha unapata taarifa sahihi kwa kufuatalia kuaminika kwa chanzo cha taarifa. Pia tumia search engine kama Google, kutafuta vyanzo vingine vya habari vinasema nini kuhusu taarifa unayodhani ni sahihi.
Linda sana utashi wako kwa kuwa huo pekee ndio mali kubwa zaidi kwa maisha yako. Ukipoteza utashi wako kwa tamaa ya mali, kufuata mkumbo n.k utajikuta unapotea zaidi.
Kuwa tayari kubadilika kuendana na mazingira na hali halisi – elimu, aina ya biashara, aina ya kazi, mahali pa kuishi, mahusiano, malezi ya watoto.
Katika nyakati tulizopo, ni muhimu sana kuufahamu na kuuishi msemo huu “ Don’t Work Hard, Work Smarter”yaani “ Usifanye tuu kazi kwa nguvu zako zote, bali fanya kazi kwa akili zaidi”.