Hivyo unajikuta na wewe umekuwa wa kuiga, umejifunza kujikataa, umejifunza kutokuangalia nini hasa unataka, bali nini haswa marafiki, ndugu na jamaa wanataka au wanategemea wewe uwe vipi. Halafu ukiitafakari hali unaona ni kama vurugu kwani hakuna anayeishi maisha yake.