Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

6034171E-BE8C-4D86-A928-4E68554E219A.jpeg
 
Safi sana. Katika Uislamu hili suala limekaaje kwa ujumla. Naonaga hakuna mbwembwe yaani maiti unabebwa na wenzio mzobe mzobe kwenye jeneza/mkeka simple tu kwenda kuzikwa. Mazishi nayo siku hizi yamegeuka kuwa sehemu ya kuonyeshea ufahari na watu wanachukua mpaka mikopo benki ili kununua majeneza ya bei mbaya na tafrija za mazishi. Ujinga!

Mi ningependa nizikwe simple kabisa kama kwa hao Wapemba. Itabidi kuandika wosia mapema [emoji1545][emoji1545]
Kwa waislam imeharamishwa kuchelewesha kuzika kwa sababu zisizo za msingi.
Pia ni haram kumzika maiti na vitu vya kidunia kama suti, saa, buti,kidani, hereni nk.
Hairuhusiwi sherehe msibani kama inavyofanyika mijini siku hizi.
Katika mazishi ya kiislam tofauti ya masikini na tajiri ni msibani, kwa tajiri huenda waombolezaji watakula pilau, kwa masikini huenda mkaenda kuzika bila kula, lakini maiti watavalishwa sanda zinazofanana, watalazwa kwenye kaburi zinazofanana na kufunikwa na ubao wa kawaida.
Utajiri au umasikini ni wakati wa uhai wako tu.
 
Back
Top Bottom