Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa waislam imeharamishwa kuchelewesha kuzika kwa sababu zisizo za msingi.
Pia ni haram kumzika maiti na vitu vya kidunia kama suti, saa, buti,kidani, hereni nk.
Hairuhusiwi sherehe msibani kama inavyofanyika mijini siku hizi.
Katika mazishi ya kiislam tofauti ya masikini na tajiri ni msibani, kwa tajiri huenda waombolezaji watakula pilau, kwa masikini huenda mkaenda kuzika bila kula, lakini maiti watavalishwa sanda zinazofanana, watalazwa kwenye kaburi zinazofanana na kufunikwa na ubao wa kawaida.
Utajiri au umasikini ni wakati wa uhai wako tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…