Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Allah Muumba mbingu na ardhi tunakuomba utujaalie kila la kheri waja wako kwenye siku hii nyingine.
Kila zito likawe jepesi, kila gumu ulipe wepesi.
YARAB Ìkinge Dunia dhidi ya maradhi mabaya ya kuambikiza na yale yasiyo ya kuambukiza.

YARAB Wasamehe wenzetu waliotangulia mbele ya haki.
Twakuomba uyafanye makaburi yao kuwa mabustani kama yalivyo mabustani ya peponi, yasiwe mashimo kama yalivyo mashimo ya motoni.

Amin[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Amin, na iwe siku njema kwetu sote [emoji120]
 
Nidhamu ya mawasiliano;
1. Piga simu mara moja tu, Kama hajapokea tuma ujumbe wa meseji.
2. Kama ni namba mpya, Tuma meseji kwanza Usipige.
3. Usikate simu kama sio wewe uliepiga
4. Usifanye maongezi mengine wakati unaongea na mtu kwenye simu.
5. Piga simu pale penye ulazima wa kufanya hivyo.
6. Ongeza yako.......
 
MIKATE ILIVYOCHANGIA KUTOKEA KWA MAPINDUZI YA SERIKALI KUBWA DUNIANI

Kama ambavyo tunasema Mama ndio hulewa familia basi tunaweza kusema kuwa MKATE NDIO UMEILEA DUNIA HADI KUFIKA HAPA TULIPOFIKIA
Ndio japo kwa sasa kinaonekana ni chakula dhalili lakin kiuhalisia mkate ni miongoni mwa vyakula vya mwanzo kutengenezwa na binadamu na kilikuwa na hadhi kubwa saaana hapo mwanzoni
Ukiachana na kwenye suala la kula lakini pia mkate umechangia kiasi kikubwa katika kutokea kwa MAPINDUZI YA UFARANSA yaliofanikiwa kumtoa kiongozi dhalimu Mfalme Louis XVI na mke wake Marie Antoinette
Unaweza kujiuliza inakuaje hivi Lakini kiukweli ni kuwa mapinduzi ya ufaransa yamechangiwa na sababu Kubwa nyingi lakin kuadimika kwa mikate ambayo ndio kilikuwa chakula cha watu wengi kiliongezea hasira kwa raia ...hata wewe usingechukua hatua ukimuona mke wa mfalme Marie Antoinette anaishi maisha ya kifahari anatumia anavyotaka ila wewe unakosa hata mkate?
Sababu kubwa ni kukosekana kwa nafaka za kutengenezea mikate hivyo mikate ikapanda bei... Kwahiyo Raia waliona serikali imeshindwa kutimiza majukumu yake
Lakini suala hili la mikate nchin ufaransa halikuwa mara ya kwanza kutokea kwan katika miaka 1529 kulitokea maandamano makubwa katika jiji la Lyon nchin ufaransa baada ya kukosekana kwa nafaka kwa ajili ya kutengenezea mikate... Maandamano hayo yakipekekea vifo vya baadhi ya watu kuvunjwa kwa maduka na hasara nyengine nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…