Kuna watu huwa hawajisikii vizuri pale sauti ya televisheni au vifaa ikiwekwa kwenye mfumo wa namba witiri.Witiri ni namba yoyote isiyogawanyika kwa mbili mfano 3,5,7,9......
Tafiti: Wanawake hutoka nje kimapenzi (Cheat) kwa sababu kubwa inayotajwa kusumbuliwa na "Upweke", Wakati Wanaume wao huwa na sababu ndogo ndogo kama kutaka heshima, kulipa kisasi au kutamani tu kufanya hivyo etc.
Tafiti: Wanaume ndiyo huongoza zaidi kutoka nje kimapenzi kuliko Wanawake, 34% ya wanawake wanaotoka nje kimapenzi (Cheat) huwa na furaha kwenye ndoa zao wakati 54% ya Wanaume wanaotoka nje kimapenzi nao huwa na furaha kwenye ndoa zao
Hart Audio D&W Aural Pleasure" ni Spika mbili zilitengenezwa na Hart Audio mwaka 2012. Zimeundwa kwa karati za dhahabu zinazofikia 24, Kuzipata bila makato ya kodi ni tsh Bilioni 11.5.
Pomboo ni wanyama wa majini wanaofanana sana na nyangumi. Inatajwa kuwa, kuna pomboo takribani aina 40. Pomboo wana ukubwa tofauti, kuanzia urefu wa mita 1.2 – 9.5 na uzito wa kilogramu 40 mpaka tani 10. Viumbe hawa wanapatikana duniani kote, hasa kwenye bahari za kina kifupi.
Pomboo huweza hata kuwasaidia wenzao kupumua kwa kuwasogeza kwenye usawa wa maji. Huko New Zealand, pomboo waliwahi kuonekana wakilinda jike na ndama wao.
Pomboo, mara nyingi, huwa Mara katika makundi. Mara kadhaa, pomboo, hasa dume, wame kuwa wakigombana na hivyo kusababisha kuwa na makovu mengi mwilini mwao. Aghalabu sababu ya kupigana ni kugombania nafasi ya kuwa na jike. Wale wanaoshindwa huenda zao mbali.
Midomo ya pomboo imechongoka na vijimeno vyake ni vidogo vidogo sana lakini hatari. Umaarufu wa samaki huyu pengine umechagizwa pia na mahusiano yake na binadamu.
Wataalamu wa elimu ya viumbe wa baharini wanasema, ni vigumu kufa maji kama pomboo yupo eneo hilo kwani samaki huyu anaweza kuja kukuokoa. Akiwepo samaki huyu jirani pia huwezi kudhuriwa na samaki wakali kama papa. Pomboo atakulinda kwa hali na mali.
Inapotokea umedumbukia majini na akakuona, haraka pomboo hukujia sana, kisha atakukumbatia na kwa spidi kubwa atakuwa anakupeleka nchi kavu. Atakapofika jirani atakurusha huko na msaada wake huishia hapo. Ukitua kwenye jiwe, mwamba, michongoma au kwenye mti hiyo ni shauri yako yeye kazi yake kashamaliza
Pomboo hujamiiana kwa vipindi vifupi lakini hufanya mara nyingi nyingi katika muda mfupi. Pomboo hubeba mimba kwa muda wa miezi 11-12, kutegemeana na aina husika. Pomboo huanza kujamiiana katika umri mdogo. Pia, umri hasa wa kukomaa kijinsia hutofautiana kutoka aina moja mpaka nyingine.
Pomboo huzaa mtoto mmoja au wawili, na huyu ni samaki mwenye kasi kubwa ya kusafiri majini. Pomboo hatagi bali anazaa. Pia, pomboo hunyonyesha. Samaki huyu anafanana na mwanadamu katika mambo mengi, ikiwemo kuzaa na kunyonyesha na vilevile kuishi kifamilia.
Pamoja na kwamba samaki ndiyo chakula chake kikuu, pomboo pia hupendelea zaidi kula pweza na fisi maji. Pomboo hula kwa namna mbalimbali na pia ana mbinu mbalimbali za kushambulia samaki.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.