Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1615744820962.png
 
Huko Urusi watu wawili mwanamke na mwanaume walipata ajali wakiwa na mbwa wao. Mwanamke alikufa hapo hapo na mwanaume aliwahishwa hospitali lakini baadae alikufa, mbwa pekee ndiye alipona. Baada ya tukio lile mbwa aliendelea kukaa eneo hilo, licha ya watu kujaribu kumchukua kutaka kumrudisha nyumbani, wengine walitaka kumchukua ili wamfuge lakini mbwa huyo alikataa kutoka kwenye eneo la ajali na akakaa katika eneo hilo hadi alipokufa miaka saba baadaye. Kutokana na kitendo hicho cha uaminifu alichokionesha mbwa huyo, lilitengenezwa sanamu kubwa la mbwa huyo na kuwekwa katika mji huo kama njia ya kuheshimu uaminifu wake
 
Mwaka 1958, msichana wa kizungu aliwabusu wavulana wawili wamerakani weusi wa miaka 9 na 7, kwenye mashavu. Baada ya tukio hilo wavulana hao wawili walikamatwa, wakafungwa kwa siku 6 bila taarifa yeyote kwa wazazi wao. Walipigwa sana na polisi na walifungwa kwa jumla ya miezi 3.
 
Mwanamume mmoja nchini India aliyefahamika kwa jina la Neelim Kumar Khaire aliweka rekodi ya dunia mwaka 1986 kwa kutumia masaa 72 kukaa katika banda moja na nyoka wa aina 72 tofauti wenye sumu kali zaidi nchini India ili kuthibitisha kwamba nyoka hawang'ati watu kama hawajachokozwa. Katika masaa hayo 72 aliyokaa katika banda ilo lenye nyoka wakali, Khaire hakuonesha wasiwasi wowote, ndo kwanza alikua anasoma magazeti na muda mwingine kusinzia kabisaa bila uwoga. Alitoka ndani ya banda ilo bila kuumia wala kuumwa na nyoka hata mmoja.
 
Mwaka 2019, polisi nchini Brazil walimkamata kasuku aliyepewa mafunzo na wafanyabiashara wa dawa za kulevya. Kulingana na ripoti, ndege huyo alikuwa amefundishwa kutoa tahadhari kwa wahalifu kuhusu polisi kwa kupiga kelele: "Mama, polisi!" Mara tu polisi wanapokaribia, anaanza kupiga kelele
 
Mwaka 2019, polisi nchini Brazil walimkamata kasuku aliyepewa mafunzo na wafanyabiashara wa dawa za kulevya. Kulingana na ripoti, ndege huyo alikuwa amefundishwa kutoa tahadhari kwa wahalifu kuhusu polisi kwa kupiga kelele: "Mama, polisi!" Mara tu polisi wanapokaribia, anaanza kupiga kelele
 
Mwaka 1721, mwanamke wa Scotland, Maggie Dickson alihukumiwa kifo kwa kunyongwa. Alining'inizwa, akatangazwa amekufa, akawekwa kwenye jeneza la mbao, na kusafirishwa. Akiwa njiani kuelekea maeneo ya kanisa alizinduka na kuonekana akiwa mzima. Kwa mujibu wa sheria ilisema adhabu yake imetekelezwa kwaio atakama ameonekana mzima (hajafa) adhabu yake imeshaisha na aliishi miaka mingine 40 ndipo akafa.
 
Mwaka 1977, Pradyumna Kumar Mahanandia, msanii wa India, aliendesha baiskeli kwa miezi minne na wiki tatu kutoka New Delhi hadi Gothenburg huko Sweden ili kwenda kukutana na mpenzi wake Charlotte Von Schedvin. Alienda kwa baiskeli kwasababu hakuwa na pesa za kutosha kununua tiketi ya ndege. Baadae Walioana na sasa wana watoto wawili
 
Mwaka 1901 huko hispania, mwanamke mmoja alichukua kitambulisho cha kiume kwa kujifanya mwanaume na kumuoa mwanamke mwenzie. Wana ndoa hao waligunduliwa baadaye sana na walipojua wamegundulika ilibidi wakimbilie Argentina. Hati yao ya ndoa haikuwahi kufutwa, kwa hivyo hii ndiyo ilikua ndoa ya kwanza iliyorekodiwa ya watu wa jinsia moja huko hispania. Miaka 100 baadae Serikali ya Hispania ilihalalisha ndo za watu wa jinsia moja.
 
Baada ya kupata homa na kufadhaika mwaka 1392, Mfalme Charles VI wa Ufaransa alianza kupatwa na wazimu (ukichaa) ambao ulidumu maisha yake yote. Mojawapo ya wazimu wake maarufu alikua anaamini kwamba mwili wake ulikuwa umeumbwa kwa vioo.😁 Mara zote alikua akiogopa na kuutunza mwili wake wa kioo usivunjike, alikua anakataa kutembe tembea, mara nyingi alikaa kwa kutulia sehemu moja kwa muda mrefu.
 
Kila mwaka watu 30,000 hukusanyika pamoja katika mitaa ya Bunyol, Hispania, kushiriki pambano kubwa zaidi la nyanya duniani. Pambano linalofahamika kwa jina la "LA TOMATINA". Kilo 125,000 za nyanya zinaletwa kupitia lori. Makombora 5 makubwa yaliyojaa nyanya yanalipuliwa angani kuanza pambano. Katika pambano hili kuna sheria mbili tu: 1) Lazima ubonyeze kila nyanya kabla ya kumtupia mwenzio kuona kama nyanya sio ngumu ili usimuumize mtu utakapomlenga. 2) Nyanya tu ndo zinazotakiwa kutupiana
 
Chung Ju-Yung, alizaliwa mwaka 1915 katika familia masikini ya kikulima huko Korea Kaskazini. Katika familia yao kulikua na watoto nane (8), yeye ndo alikuwa mtoto mkubwa kuliko wote. Huyu ndiye mwanzilishi wa Kampuni ya Hyundai. Enzi izo akiwa kapuku (hana pesa) kabla ya kuanzisha Hyundai, alikua anaishi kijijini kwao uko Asan, alifanya majaribio matatu kukimbilia Korea Kusini lakini hakufanikiwa, Baba yake alimkamata na kumzuia. Hatimaye alifanikiwa mara ya 4 baada ya kuiba ng'ombe mmoja wa baba yake na kumuuza kwa pesa ambazo zilimsaidia kupata usafiri wa gari moshi (treni) hadi Seoul. Kipindi hiko alikuwa na miaka 16 tu. Baadaye mnamo 1998, alituma ng'ombe 1001 kijijini kwao huko Asan, Korea Kaskazini kama malipo ya ng'ombe mmoja aliyeiba na kumuuza ili aweze kununua tiketi ya gari moshi (treni).
 
Huko nchini Scotland kuna kisiwa kinajulikana kama Kisiwa cha Majadiliano. Kihistoria katika kisiwa hiki watu wale ambao walikuwa na mabishano au ugomvi walipelekwa kwenye kisiwa na kuachwa peke yao, wanaachiwa jibini na whisky. Lengo la kupelekwa kwenye kisiwa hiki ni ili watu waweze kutatua shida zao wenyewe na ilikua hawawezi kuondoka hadi watakapofikia muafaka na kuelewana wote wawili. Inaaminika kisiwa hiki kimetumika kwa namna hii kwa takribani miaka 1500 au zaidi, na katika miaka yote hiyo iliwahi kutokea kesi moja tu ya mtu kuuwawa akiwa huko
 
Hahahahahaha mie na familia yangu hata siku moja hatujawahi kuunga mkono udhalimu kwa Mtanzania yoyote yule bali ni TUNAPINGA TU TENA KWA NGUVU ZOTE!!

Hio karma iwe juu yako na familia yako
 
Back
Top Bottom