Chung Ju-Yung, alizaliwa mwaka 1915 katika familia masikini ya kikulima huko Korea Kaskazini. Katika familia yao kulikua na watoto nane (8), yeye ndo alikuwa mtoto mkubwa kuliko wote. Huyu ndiye mwanzilishi wa Kampuni ya Hyundai. Enzi izo akiwa kapuku (hana pesa) kabla ya kuanzisha Hyundai, alikua anaishi kijijini kwao uko Asan, alifanya majaribio matatu kukimbilia Korea Kusini lakini hakufanikiwa, Baba yake alimkamata na kumzuia. Hatimaye alifanikiwa mara ya 4 baada ya kuiba ng'ombe mmoja wa baba yake na kumuuza kwa pesa ambazo zilimsaidia kupata usafiri wa gari moshi (treni) hadi Seoul. Kipindi hiko alikuwa na miaka 16 tu. Baadaye mnamo 1998, alituma ng'ombe 1001 kijijini kwao huko Asan, Korea Kaskazini kama malipo ya ng'ombe mmoja aliyeiba na kumuuza ili aweze kununua tiketi ya gari moshi (treni).