Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Huko nchini Mexico kuna kisiwa kinachojulikana kama "La Isla de las Muñecas" yaani kisiwa cha midoli. Jina hili limetokana na uwepo wa midoli mingi ya ajabu ajabu iliyoning'inizwa kwenye miti ya eneo ilo. Simulizi hii inahusishwa na Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Don Julian ambaye ndiye alikua anaishi eneo ilo. Don Julian alidai kuwa kisa cha kuning'iniza midoli hiyo katika miti kilianza muda mfupi baada ya kuhamia katika kisiwa hiko, alikutana na tukio la kutisha, alikuta mwili wa msichana mdogo ufukweni mwa kisiwa, na muda mfupi baada ya tukio hili, Don Julian aliona mdoli akielea majini karibu na alipokuta mwili wa mtoto yule. Kwa kuwa alikuwa akiishi kisiwani peke yake, Don Julian alichukua mdoli yule, akamtundika juu ya mti kama njia ya kutuliza roho ya msichana yule mdogo aliyekufa. Lakini hakuishia hapo miaka iliyofuata aliendelea kutundika midoli ya kila aina. Don Julian muda mwingine alikua akiokota midoli iliyotupwa jalalani na kuwatundika kwenye miti kisiwa chote. Alikua hachagui mdoli wa kuokota, aliokota vipande vya mdoli, visivyo na kichwa, miguu, macho yote aliokota. Kwa kawaida ni midoli ambayo inatisha ukiitazama. Watu wengi walimuona kama ana matatizo ya akili hawakuamini kuhusu hadithi yake kuhusu msichana mdogo aliekufa, waliona ni kama hadithi ya kutungwa tu aliyoianzisha. Lakini jambo la kutisha katika hadithi hii ni jinsi mwisho wa maisha yake unavyoungana moja kwa moja na hadithi ya msichana mdogo aliyekufa. Don Julian alikufa 2001. Mwili wake ulikutwa sehemu ile ile ambayo kila wakati alidai kuwa alikuta mwili wa msichana mdogo amekufa.
 
Mwaka 1714, Meli 2 za kivita zilizokuwa zikiongozwa na Wessel na Bactmann, zilipigana kwa masaa 14, hadi meli moja ilipoishiwa silaha. Nahodha wa Meli iliyoishiwa silaha alikuwa ni Wessel, alimtumia ujumbe mpinzani wake, kumshukuru kwa mpambano mzuri na kuomba kupewa silaha zaidi, ili pambano liendelee. Bactmann alikataa, lakini aliamua kuondoka na kumuacha mpinzani wake bila kumshambulia licha ya kuishiwa silaha. Wessel alihukumiwa mahakamani kwa vita hii ya kiungwana kwa kosa la kutoa siri ya kuishiwa silaha kwa adui yake lakini baadae aliachiwa huru na kisha kupandishwa cheo kuwa Kapteni
 
Mwaka 1811, Tecumseh, kiongozi wa jadi marekani na vijana wake walikabiliwa na jeshi la marekani likiongozwa na William Henry Harrison. Vita vilipigwa katika Mto Tippecanoe na kumalimalizika kwa kushindwa kwa Tecumseh na kusababisha kifo cha kaka yake, Tenskwatawa. Vita hiyo ilitokana na kutetea eneo lao dhidi ya upanuzi mkubwa wa ardhi wa Marekani hadi magharibi. Tecumseh alikufa miaka miwili baadaye katika Vita vya Thames alipokua akiwasaidia Waingereza kupambana na Wamarekani.
 
Hapa ndo patamu sasa👇 Kulingana na simulizi, Tecumseh alitoa laana ambayo imewasumbua wamarekani kwa takribani miaka 200. Laana ilikuwa kwamba kila rais wa Marekani atakaechaguliwa katika mwaka unaogawanyika na ishirini na kuishia na sifuri atakufa kabla ya kumaliza kipindi chake. Laana hii ilidhihirika mwaka 1841 wakati William Henry Harrison alipokufa kwa homa ya tumbo (typhoid) miezi michache baada ya kushinda uchaguzi mwaka 1840. Tangu wakati huo, laana hiyo hiyo ilipewa jina la "Laana ya Tippecanoe" au "Laana ya Tecumseh,"
 
Marais wengine waliokumbwa na laana hii ni 👇 Abraham Lincoln, alichaguliwa mwaka 1860 na kuuawa mwaka 1865. James A. Garfield alichaguliwa 1880, mwaka 1881 akapigwa risasi na kufa baadaye mwaka huo huo. William McKinley alichaguliwa tena mwaka 1900. Alipigwa risasi mwaka 1901 na kufa wiki moja baadaye. Warren G. Harding, aliyechaguliwa mwaka 1920. Alikufa kwa mshtuko wa moyo mwaka 1923. Uvumi unasema alilishwa sumu na mkewe. Franklin D. Roosevelt, aliyechaguliwa tena mwaka 1940 kwa kipindi cha tatu, alipata kiharusi na kufa baada ya miezi 3 kuingia muhula wake wa nne mwaka 1945. John F. Kennedy alichaguliwa mwaka 1960. Aliuawa mwaka 1963. Ronald Reagan alichaguliwa mwaka 1980 lakini aliepuka kifo baada shambulio la risasi ya John Hinkley iliyomkosa kwenye moyo mwaka 1981. George W. Bush alichaguliwa mwaka 2000, nae 2005 alikumbana na jaribio la kushambuliwa. Ni Ronald Reagan na George Bush pekee ndio walionusulika kifo kutoka katika laana hii. Mjadala kwa Sasa ni "Je, rais mteule wa Marekani 2020 bwana Joe Biden atafanikiwa kuepuka laana hii?"
 
Joseph Michael Palmer aliyeishi kuanzia miaka ya 1789 hadi 1873, alikuwa ni mtu ambae ana mandevu mengi sanaa kama anavyoonekana pichani👆. Sasa bwana watu wa kijiji alichokua anaishi walikua wanachukia sana ndevu zake kipindi iko fashion ya kufuga ndevu nyingi haikuwepo, mara kwa mara walikua wanamwambia anyoe lakini alikataa. Wengine walikua wanamwambia kama hataki kunyoa basi wasimuone mtaani kwasababu anatisha kama shetani.😁 Siku moja mwaka 1830, Wanaume wanne wakiwa na mkasi na wembe walimvamia Palmer nje ya hoteli ya Fitchburg na kujaribu kutaka kumnyoa ndevu zake. Palmer alifanikiwa kujitetea dhidi ya watu hao. Katika pulukushani za kujitetea Palmer aliwajeruhi miguuni wawili miongoni mwa wavamizi wale. Kwa kitendo icho Palmer, alishtakiwa kwa "shambulio lisilokuwa na sababu", 😁 Palmer alishtakiwa siku chache baadaye mbele ya Jaji David Brigham na kupigwa faini. Palmer alikataa kulipa faini ambayo ilitokana na kuhukumiwa kwake kwa uhalifu wa kujitetea. Palmer alitupwa jela kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa kukataa kulipa faini hiyo.
 
Johanna Quaas amezaliwa Novemba 20, 1925 huko Hohenmölsen ni mtaalam wa mchezo wa mazoezi ya mwili wa Ujerumani (gymnasty/ gymnastic). Gymnastic ni mchezo ambao unajumuisha mazoezi ya mwili yanayohitaji usawa (balance), nguvu, kubadilika(flexibility), wepesi, uratibu (coordination) na uvumilivu. Johanna Quaas ndiye mshiriki wa mchezo huu mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani. Novemba 20 mwaka huu anatimiza miaka 96.
 
Kama ulikua haufahamu ndo ilikua hivi Sasa 👇 Huko Uingereza, katikati ya miaka ya 1960 kabla ya kuwepo kifaa cha kupimia mimba, vipimo vya ujauzito vilifanywa kwa kuingiza mkojo wa mwanawake kwa chura na kuangalia ikiwa kama atataga mayai ndani ya masaa kumi na mbili. Kama akifanikiwa kutaga basi mwanamke mwenye huo mkojo ana mimba. Yote hii ilifanyika katika maabara. Kipimo cha kwanza cha upimaji wa ujauzito kilitengenezwa mnamo mwaka 1971 ambacho mwanamke angeweza kupima mkojo wake mwenyewe na kungoja kwa masaa mawili ili kuthibitisha.
 
Ningekuwa kichaa ningemuunga mkono huyo dhalimu kama taahira wewe mwenye roho mbaya ya kutisha usiyekuwa na UTU hata chembe. Maovu wanayotendewa binadamu wewe kwako ni furaha tele.
Who knows kichaaa
 
Mwaka 2019, Elizabeth Hoad, mwanamke wa Uingereza mwenye umri wa miaka 49, aliolewa na mbwa wake. Alielezea kuwa alifikia uhamuzi huo baada ya kuchumbiwa mara nne na kujihusisha kwenye mapenzi na wanaume 220 bila kuolewa. Hivyo amechoshwa na binadamu (waanaume) na kuamua kuolewa na mbwa wake aliyefahamika kwa jina la Logan. Kwa upande wake anaona kuolewa na mbwa wake amejiokoa yeye pamoja na mbwa kutoka kwenye upweke.
 
Asante kwa habari hizi
 
Tim Friede, mwanasayansi kutoka Wisconsin, Marekani. Huyu ni binadamu asiyedhulika na sumu ya nyoka wa aina yoyote. Ameng'atwa na nyoka wa aina tofauti tofauti zaidi ya mara 200 katika miaka 20. Amevumilia hata kuumwa na Black Mamba wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambae inaaminika ni miongoni mwa nyoka wenye sumu kali zaidi duniani
 
Asante kwa habari hizi
 
Mwaka 2019, wakati jiji la Bhopal, India, lilipokumbwa na ukame, makuhani wa huko waliwafungisha vyura wawili ndoa ili kumuomba Mungu wa mvua awape mvua. Kwa bahati mbaya, ndoa ya vyura hao ililazimika kuvunjwa miezi michache baadaye ili kuzuia mvua kuendelea kwa sababu ya mvua kubwa iliyoendelea kunyesha ambayo ilisababisha uharibifu wa nyumba zaidi ya 9,000
 
Familia ya ndugu 12 nchini Canada ilishinda Rekodi ya dunia ya Guinness (Guinness world record) kwa familia yenye umri mkubwa zaidi wa ndugu wanaoishi. Umri wa pamoja wa ndugu hao, ambao ni familia ya dada tisa na kaka zao watatu, ni miaka 1042 na siku 315, na umri wao ni kati ya miaka 75-97. Ndugu hawa wote walizaliwa tumbo moja (ndugu wa baba mmoja na mama mmoja) huko Pakistan.
 
Los Maniceros massacre ni tukio baya la mauwaji lililotokea mwaka 2009 nchini Colombia lililohusisha utekwaji wa wachezaji 12 wa timu ya mpira wa miguu ya Los Maniceros ambao waliteswa kwa muda wa wiki mbili na baadaye kupatikana wamefariki msituni huku mmoja pekee akipona. Miili ya wachezaji hao wote 11 waliokufa ilipatikana msituni huko mipakani Táchira Venezuela umbali wa zaidi ya kilomita 600 kutoka Colombia wiki mbili baada ya kutekwa. Kwa mujibu wa mchezaji Manuel Cortez wa umri wa miaka 19 aliyepona katika tukio hilo baada ya kukimbia alisema kuwa baada ya yeye na wenzake kutekwa walifungwa minyororo shingoni kwenye miti na kuachwa kwa muda huo wa wiki mbili huku yeye akifanikiwa kutoroka akiwa amepigwa risasi shingoni. Ilikua ni October 11, 2009 mjini La Tala mpakani mwa Colombia na Venezuela ambapo wachezaji hawa walikuwa njiani kutoka kwenye mechi, wakatekwa na watu wasiojulikana na kupelekwa mbali, walipatikana wakiwa wamekufa Oktoba 24, 2009. Licha ya uchunguzi mkubwa kufanyika lakini hakukuwa na majibu ya moja kwa moja yaliyotolewa na serikali juu ya chanzo au washukiwa wa mauwaji hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…