Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Huko nchini Scotland katika miaka ya 1500's - 1600's kulikuwa na mtu hatari sana aliyejulikana kama Alexander "Sawney" Bean. Maisha aliyokuwa anaishi huyu jamaa ni ya kutisha haijawahi tokea, alikuwa anamiliki watu, yaani kama jinsi watu wanavyomiliki mifugo kama kuku, n'gombe au mbuzi basi ndivyo jamaa naye alivyokuwa anamiliki watu. Nikizungumzia watu katili niliowahi kuskia simulizi zao hapa duniani, basi huyu jamaa nimemvulia kofia. Bean alikufa kwa kunyongwa kutokana na makosa ya kuwafanya binadamu wenzake nyama huku akiwa ameacha jumla ya watoto 29. Kwa zaidi ya miaka 25 aliyaishi maisha hayo ya kinyama mapangoni mjini East Lothian. Alikuwa ameshawafanya nyama watu zaidi ya 5,000 na wengine bado walikutwa amewafungia. Baada ya Bean kuhama nyumbani alienda kuishi mapangoni na mkewe Agnes Douglas huko Bennane Head nchini humo ambako katika maisha yao walifanikiwa kupata watoto sita, baadaye familia ikakua na kufika wanafamilia 45, hakuna aliyekua anajua mapangoni humo kama kuna watu wanaishi. Yeye pamoja na wanawe walianza kuteka watu, wanawafungia mapangoni humo alafu wanawachinja na kuwala nyama kama jinsi tunavyokula mifugo yetu nyumbani. Mabaki walikua wanayatupa ufukweni hali iliyopelekea watu kuamini kuwa kulikuwa na wanyama wakali wanaokula watu, hawakujua kabisa kama kuna familia inaishi katika mapango hayo yaliyopo karibu. Bean na familia yake hiyo kubwa waliendelea kufanya uhalifu huo hadi siku moja walipomvamia bwana mmoja aliyekua mjuzi kupigana, baada ya kuwadhibiti maadui akawapeleka kwa viongozi, ikabidi waongozane hadi mapangoni wakiwa na kikundi cha askari 400 wa mfalme James VI. Kufika mapangoni walistaajabu kuuona ukoo mkubwa wa Bean ukiishi humo, mabaki ya miili yalikuwa mengi mnoo huku sehemu nyingine zikining'inizwa ukutani, miili iliyopatikana mapangoni humo kwa siku hiyo ilifika 1000, wengine walikuwa wamefungwa wakiwa wazima. Bean alikamatwa na kunyongwa siku hiyo
 
Alifahamika kama Shi Gulan, lakini watu wake wa karibu walimbatiza jina la Shi Jianqiao kumaanisha 'Upanga' unaoashiria ahadi yake ya kulipiza kisasi kifo cha babake aliyeuawa kwa kukatwa kichwa na kiongozi Sun Chuanfang, mwaka 1925. Shi Jianqiao alitumia miaka 10 kulipiza kisasi kifo cha babake. Miaka kumi baada ya Sun Chuanfang kustaafu, Shi Jianqiao, alimvizia na kumuua kwa kumpiga risasi kichwani akiwa anaomba katika hekalu la kibudha . Badala ya kutoroka eneo la tukio, Shi Jianqiao aliamua kubaki na kuwasimulia wapita njia kuhusu kitendo alichofanya. Inadaiwa hatua hiyo ilikuwa njama ya kuvutia vyombo vya habari na kutafuta huruma ya watu. Alifikishwa mahakamani na kusamehewa mashtaka mwaka 1936 kwasababu kosa lake lilionekana kama kisasi halali cha wazazi wake. Shi Jianqiao alifariki mwaka 1979 akiwa na miaka 73
 
Mwaka 2012, kamanda wa Taliban wa Afghanistan Mohammad Ashan alikua anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kupanga mashambulizi ya kigaidi, yakabandikwa mabango yanayoonesha sura yake na kutangazwa zawadi ya dola $100 (230k ya sasa) kwa atakaefanikisha kumkamata. Jamaa baada ya kuona hivyo alijipeleka polisi mwenyewe na kudai apewe zawadi ya $100 ambayo ilikua imeahidiwa kwenye bango la kukamatwa kwake
 
Whangamomona ni mji mdogo unaopatikana huko New Zealand Mji wa Whangamomona ulijitangaza "jamhuri" mnamo 1989, wakati huo mipaka ya kikanda ilikua inabadilishwa na mji huo ukawa sehemu ya Mkoa wa Manawatu. Mji huo umetawaliwa na rais tangu wakati huo na hufanya uchaguzi kila baada ya miaka miwili. Marais wa Whangamomona
 
IAN KJESTRUP (1989-1999) Alikua rais wa kwanza wa Whangamomona baada ya kupigiwa kura bila yeye kujua, Kjestrup alihudumia kama rais kwa miaka
 
BILLY GUMBOOT Mbuzi (1999-2001) Gumboot alikuwa mnyama wa kwanza aliyechaguliwa kuwa rais. Alishinda uchaguzi kwa kishindo, ingawa wakazi wengine wanahisi alikula kura za wapinzani wengine ili ashinde. Alifariki ofisini baada ya kutumikia kwa miez
 
TAI THE POODLE (mbwa)(2003-2004) Tai alistaafu baada ya kushambuliwa, lakini wengine hudhani ilikuwa jaribio la kumuua. Ingawa alinusurika shambulio hilo, Tai aliachwa hafai kwa huduma (alijeruhiwa vibaya)na alikufa mnamo 2010
 
SIR MURT "MURTLE TURTLE" KENNARD (2005-2015) Mmiliki wa karakana ya eneo hilo alipata ushindani mkali kutoka kwa Rais wa zamani Kjestrup na kuchaguliwa kuwa Rais wa 4. Alichaguliwa tena mnamo 2009 kwa kura moja. Kennard alikufa katika Hospitali ya New Plymouth mnamo 25 Oktoba 2015.
 
VICKI PRATT (2015–2017) Pratt alikuwa Rais wa kwanza mwanamke aliyeteuliwa katika Jamuhuri ya Whangamomona. Alichaguliwa wakati alikuwa akifanya kazi jikoni.
 
JOHN HERLIHY (2017- sasa) Herlihy alichaguliwa na kuwashinda wake Jack Spearow, Lili Jiao na Ted. Licha ya kuripotiwa kuwa Spearow aliiiba kura, siku ya Jamhuri 2019 (Januari ya tarehe19) Rais Herlihy alichaguliwa tena kwa muhula wa pili, baada ya kupambana na changamoto nyingi kutoka kwa wapinzani wake.
 
Mnamo mwaka 1999 mbuzi kwa jina Billy Gumboot alichaguliwa kuwa rais katika eneo la Whangamomona nchini New Zealand. Mbuzi huyu alishinda uchaguzi kwa kula kura za wapinzani wengine. Alifariki ofisini baada ya kutumikia kwa miezi 18 kuanzia 1999 - 2001. Najua unajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu😂😂
 
Kwa wale wenye tatizo la kukosa Usingizi suluhisho ni kunywa mchanganyiko wa maziwa na asali. Chukua glasi ya maziwa kisha changanya na asali kijiko kikubwa na unywe kabla ya kulala.Utapata usingizi mnono.
 
Mnamo mwaka 1999 mbuzi kwa jina Billy Gumboot alichaguliwa kuwa rais katika eneo la Whangamomona nchini New Zealand. Mbuzi huyu alishinda uchaguzi kwa kula kura za wapinzani wengine. Alifariki ofisini baada ya kutumikia kwa miezi 18 kuanzia 1999 - 2001. Najua unajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…