Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Woo Bum-kon alikuwa polisi wa Korea Kusini, Mwaka 1982, Usiku wa Aprili 26 hadi Aprili 27 aliua na kujeruhi watu katika vijiji kadhaa uko Uiryeong, Korea Kusini kisha baadae kujiua. Kabla ya kutekeleza mauaji hayo Woo alikua amegombana na mpenzi wake ambaye alimwamsha kutoka usingizi kwa kumpiga kofi la kifuani alipokua anamfukuza nzi wakati Woo amelala mida ya mchana. Kitendo hicho kilimkasirisha akaondoka nyumbani na kwenda kazini, Baadae jioni alirudi nyumbani na kuanza kumpiga mpenzi wake na kuvunja vunja vitu vya ndani. Hasira za Woo hazikuishia hapo alienda kuchukua silaha Katika sehemu ya kuhifadhia silaa akaingia mtaani na kuanza kuua watu mtaa mmoja hadi mwingine, aliua watu 56 na kujeruhi wengine 35 kisha na yeye akajiua.
 
Mwaka 1898 ilichapishwa riwaya ya "Futility" iliyoandikwa na Morgan Robertson ambayo ilipata umaarufu zaidi kuanzia miaka ya 1912 baada ya kuzama kwa Meli ya Titanic na kubadilishwa jina na kuitwa "The wreck of the Titan". Riwaya hii iliyokuwa imeandikwa miaka 14 kabla ya kuzama kwa Meli ya Titanic ilipata umaarufu na kuonekana kama mwandishi alitabiri kilichotokea katika kuzama kwa Meli ya Titanic kutokana na mfanano wa mambo mengi yaliyoelezewa kwenye riwaya na uhalisia wa kuzama kwa meli hii pamoja na kuendana kwa ukubwa wa Meli hizi na ata pia katika riwaya ilielezea Meli kuzama mwezi April na baadae baada ya miaka 14 kupita katika uhalisia Meli ya Titanic ilizama pia April 1912.
 
Mnamo July, 1518 wakazi wa mji wa Strasbourg walikumbwa na ugonjwa wa ajabu wa kucheza mfululizo bila kupumzika! Picha lilianza kwa mwanamke mmoja anaejulikana kama Frau Troffea alipoingia mtaani na kuanza kucheza kwa siku sita mfululizo. Baadae kundi kubwa la watu likajumuika na kuanza kucheza kiajabu ajabu yaani dansi isiyoeleweka. Mpaka kufika Agosti, ugonjwa huu ulikuwa umeshawakumbuka watu wapatao 400 na kukiwa hakuna majibu nini haswa kimetokea kwa wakazi hao, baadhi ya wataalamu wakadai ni kuchemka kwa damu na kuwa ya moto "hot blood" na kusababisha stress iliyopelekea mwili kufanya vitu vya ajabu/hatari bila hiari yako. Jitihada za serikali zilipelekea kujengwa kwa jukwaa maalumu na kuwaita wataalamu wa muziki ili waweze kuwapigia mziki pengine ugonjwa huo ungetoka lakini hawakufanikiwa. Watu walianza kuanguka na kufa kutokana uchovu mwingi. Wengine walikufa kutokana na magonjwa ya moyo na stroke. Kisanga hiki kiliendelea mpaka Septemba pale ambapo wanakijiji walienda milimani na kuanza kuomba ili kuyashinda yanayowasibu. Kisa kama hiki kilishawahi kutokea huko Uswisi, Ujerumani, na Uholanzi lakini haikuwa babu kubwa kama hii ambayo ilichukua uhai wa watu.
 
Duh...
 
Aisee
 
Duh...
 
Mwaka 1942, Mwanaume aliyepewa jina la Phantom Barber alikua anavunja na kuvamia nyumba za watu huko Mississippi na kukata nywele zao. Alikuwa anakata nywele za wanawake hususani wasichana wadogo. Uvamizi huo alikuwa akiufanya wakati wa Usiku pindi watu walipokuwa wamelala. Licha ya kuwepo kwa kesi nyingi za watu kukatwa nywele lakini muhusika hakuweza kutambulika ni nani. Siku moja alivamia katika nyumba moja ambayo ilikuwa wanaishi mke na mume ambapo baada ya kushindwa kutimiza lengo lake aliwadhulu kwa kuwapiga na bomba la chuma. Tukio hili la kuwashambulia wanandoa lilichochea hisia za watu na msako wa kumtafuta Phantom Barber uliongezeka, mwishowe mtuhumiwa alipatikana. Mwanamume aliyeitwa William Dolan alikamatwa na kushtakiwa kufanya jaribio la mauaji. Nywele za kibinadamu pamoja na bomba la chuma lililotumika katika shambulio lilipatikana karibu na nyumba yake, lakini hakukubaliana na mashitaka hayo ambayo baada ya uchunguzi kufanyika ilikutwa hana hatia hivyo akaachiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…