Na nakumbuka katika majarida ya wakati ule "African Events", kaka yetu Ahmed Rajab aliandika makala akimuelezea Maalim Seif kama kiongozi, alimpa sifa za "Young, dynamic, vibrant and visionary", (kijana mwenye nguvu ya kutenda, hamihiri mwenye maono) kwahiyo alituvutia wengi wakati huo tupo kwenye maskuli, na ulipokuja mvutano, yaani zilipokuja siasa mpya za awamu ya tatu, walikuwepo wapinzani ndani ya chama kimoja cha CCM. Waliokuwa wakipingana na siasa zile za kimaendeleo wakitaka tubaki kule kule tulipotoka.