Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mimi nakumbuka alipokuja Chief Emeka Anyaoku mwaka 1996 baada ya uchaguzi wa mwanzo wa mwaka 1995, na akaleta package yake ambayo alitaka iwe ndio chanzo cha mazungumzo kupitia shuffling diplomacy kwa maana ya kuwa hakukuwa na mazungumzo ya moja kwa moja, yaani alikuwa anaenda kuzungumza na CCM na baadae anakuja kuzungumza upande wetu sisi tukiwa CUF.
 
Basi package ile watu wengi waliona kwamba haiakisi kabisa madai yetu kwamba sisi ni washindi wa uchaguzi wa mwaka 1995. Na tuliona kama ile ni jitihada ya kutaka kuisafisha serikali na kumhalalishia ushindi ambao haukuwa wake Dr. Salmin Amour. Lakini Maalim Seif tafauti na sote, yeye aliona fursa, na kwasababu alikuwa anaamini katika kuleta pamoja watu akasema tumepata pa kuanzia, haikuwa kazi nyepesi.
 
Nakumbuka kikao cha kamati kuu ya chama wakati ule, mimi wakati huo nikiwa katibu tu katika kuweka kumbukumbu katika vikao vya katibu mkuu, lakini nakumbuka jinsi gani alisimama kidete na kujenga hoja ya kwanini tunapaswa kukubali hatua ile ya mwanzo kuelekea katika muafaka, na ilichukua miaka mitatu 1996 mpaka 1999, disappointments zilikuwa nyingi, khiana zilikuwa nyingi sana upande wa CCM, mnakubaliana hili kesho CCM wakirudi wamelikataa, na wamekuja na mengine kabisa na tulikuwa tunekubaliana, hamfiki mwisho, lakini Maalim hakukata tamaa, akaongoza watu, hadi ukapatikana muafaka wa mwanzo.
 
Na hata pale ambapo haukutekelezwa pamoja na hayo machache yalokuwemo, bado hakuyumba katika kuamini katika ile dhana ya kuwaleta watu pamoja. Lakini hata muafaka wa mwaka 2001 ambao muafaka ule ulikuja baada ya kuuwawa Wazanzibari baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 na maandamano ya 2001, yalitokea baada ya sisi kukubaliana kuwa hakutokuwa na maandamano kwa kusema njia hii inaweza kugharimu maisha ya watu kama ilivyokuwa kawaida ya Maalim Seif siku zote alikuwa akijali maisha ya watu.
 
Lakini baadae wakati tumesafiri kwenda kufanya kampeni ya kidiplomasia juu ya yale yaliyotokezea, huku nyuma maamuzi yakabadilishwa. Lakini baada ya watu wote viongozi baada ya matokeo yale labda walijificha wengine walikuwa na khofu zao, yeye jabari la kisiasa aliamua kukatisha ziara ile, tulikuwa Uingereza pamoja, akasema yeye anarudi.
 
Akapita Nairobi kuanza kuonana na waliokuwa wakimbizi, lakini ndie wa mwanzo kupokea hoja ya kuanzisha mazungumzo ya muafaka baada ya kutolewa wito wa mazungunzo wakati watu wake wote wanampinga. Na itakumbukwa mkutano alioufanya Mnazi Mmoja, na Prof. Abdulsharif alikuwa akisema siku zote, katika mikutano yote ya Maalim Seif hajawahi kuhudhuria mkutano mgumu kwake kama ule kutokana na yaliyotokezea lakini bado akakubali mazungumzo ya muafaka ili kuunganisha watu kuipa nchi amani na kusonga mbele.
 
Na yalipokuja maridhiano vile vile, nakumbuka tulipokwenda hadharani mara ya mwanzo katika viwanja vya Demokrasia pale Kibanda Maiti mjini Unguja, Maalim Seif anazungumza hoja ya kumtambua raisi Karume ili kuweka mwanzo wa msingi wa maridhiano, watu walimzomea kwa mara ya mwanzo, kumtukana na hata kurembea vitu juu ya jukwaa lakini hakurudi nyuma.
 
Nakumbuka kulikuwa na viongozi wenzetu ambao waliyumba, na ndio hao baadae walishindwa kusimama na sisi na wakatoka kwasababu ya kutokuwa na misimamo wakafanya waliyoyafanya, lakini waliporudi walitaka kumtikisa maalim Seif katika kikao cha tathmini tulichokifanya katika ukumbi wa Mazsons.

Na wakamwambia kuwa leo yamekufika haya Unguja, kesho ukienda Pemba ukiyazungumza haya utapata fadhaa kubwa zaidi na unaweza kupigwa mawe.
 
Na la mwisho hili la juzi mnakumbuka sisi wengine tulikuwa katika vitanda vya hospitali tukiuguza majeraha, lakini alipochukua hoja ile ya kuingia katika serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa mara nyengine tena, watu wamemlaumu mno, lakini hatimae nadhani kama ni ushahidi wa faida ya yale wamekuja kuiona, na kila mmoja hata wale waliompinga walikuja kukubali kuwa Maalim aliona mbali.
 
Kwahiyo siku zote Maalim amekuwa akisimamia anachokiamini, hata kama dunia nzima itampinga akiamini yeye kuwa hichi ni sahihi anasonga mbele.

Na sote akituasa, mara moja mimi aliwahi kunambia,
"Ismail unapoambiwa wewe ni kiongozi basi kazi yako ni kuongoza, sio kufuata tu maslahi ya wafuasi kwasababu upepo unawapeleka huku ukaenda nao, kesho upepo ukiwapeleka kule ukaenda nao, wewe utakuwa sio kiongozi, wewe utakuwa ni mfuasi wao.

Wao wamekubali wewe uwe kiongozi kwasababu wamekubali your sense of judgement na kukubali kuwa wewe unaweza kuona mbali kwa maslahi yao." Na hili Maalim Seif alilisimamia.
1615742422008.png
 
1615742862317.png

Maziko ya Marehemu Bregedia Jenerali Yussuf Himid Maftah mwaka 1984. Maalim Seif Sharif Hamad yupo mkono wa kushoto kwenye picha, akifuatiwa na Mzee Ali Hassan Mwinyi, Balozi Salim Ahmed Salim yupo mkono wa kulia kwenye picha wa mwisho kulia ni Himid Yussuf Himid.

Picha na maelezo kwa khisani ya Mansoor Yussuf Himid
 
enzi hizooooo

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi-CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chama hicho Mhe. Ismail Jussa, wakiwa katika sehemu ya VIP ya uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, kwa ajili ya ziara muhimu ya chama nchini Marekani na Canada. Safari hii ni ya mwanzo kwa Maalim Seif tokea kufutwa kwa matokea ya uchaguzi halali uliomalizika Oktoba 25.
1615743316832.png
 
1615743363504.png

akili kichwani mwako

Marafiki wa miaka mingi, Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri Mkuu mstaafu na mwanadiplomasia anayeheshimika duniani, Dk. Salim Ahmed Salim, wakiwa wamekutana Uwanja wa Ndege, mjini Dar es Salaam muda mfupi uliopita.

Maalim Seif anaelekea Uingereza kuanza awamu ya pili ya ziara yake ya nchi za nje wakati Dk. Salim yeye anaelekea Zanzibar.
 
Back
Top Bottom