Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1615743518675.png
 
DOWN MEMORY LANE: Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume akikagua kikosi cha timu ya Malindi Sports Club wakati wa mojawapo ya mchezo wa mpira wa miguu uliohusisha timu hiyo katika miaka ya 60. Picha kwa hisani ya Klabu ya Malindi.

Wanaoonekana kwenye picha ni Marhoom Mzee Karume, Mohamed Qassim, Marhoom Seif Rashid, Saad Hilal Barwani na Marhoom Maalim Seif Nassor Mohamed. Hii ilikuwa mwaka 1964. Maelezo haya ya ziada ya majina ya waliomo kwenye picha na mwaka iliopigwa yametolewa na Sayyida Thubayta Bint Seif.
1615743695470.png
 
bado nipo kwenye page ya jussa nafukua vya zamani
ukitaka kumfahamu marehemu maalim seif nje ya nyumba yake, mtafute jussa
ndani ya nyumba yake, mtafute bi awena
dah hii picha ya marehemu wawili
Mungu awalaze pema huko waliko, awape pumziko bora jannat(peponi)
===================
NILIPOPATA FURSA YA KUONANA NA BALOZI AUGUSTINE MAHIGA MARA YA MWANZO

Leo wacha niwape simulizi kidogo.
Kama wananchi wengine wengi, jana asubuhi nilishtuka nilipoona Taarifa ya Ikulu ikitujuza habari za kifo cha ghafla cha Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dr Augustine Mahiga. Siyo kwamba kifo ni jambo la ajabu. Hapana, kifo hakiwezi kuwa jambo la ajabu maana sote tutakufa. Kinachoshtua siku zote huwa ni mazingira ya kifo. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa zilipotujia taarifa za msiba huu.
1615744146080.png
 
Wakati nasoma taarifa ile, hisia zangu zikanirudisha kwenye kumbukumbu zangu za miaka 16 iliyopita katika Jiji la New York.

Kwa takriban miezi mitatu kati ya mwezi Februari na mwezi Aprili, mwaka 2004 mimi na Maalim Seif Sharif Hamad tulifanya ziara refu ya kikazi katika nchi takriban 13 ikiwemo Marekani, Canada na nchi za Ulaya Magharibi. Wakati huo Maalim Seif alikuwa Katibu Mkuu wa CUF na mimi nilikuwa ndiyo kwanza nimeteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Haki za Binadamu wa CUF ikiwa ni baada ya Mkutano Mkuu wa Chama uliofanyika mwezi Februari 2004.
 
Ziara kama hizi zilikuwa zikifanyika kwa hisani na mchango mkubwa wa wananchi wenzetu wanaoishi katika nchi tunazokwenda. Hawa mara nyingi wakitulipia tiketi ya kutoka nchi moja waliopo kwenda nchi nyengine mpaka tukamaliza ratiba tuliyoipanga. Hawa pia wakitufungulia nyumba zao na kutukirimu kwa kutupatia pa kuweka ubavu, kutupatia chakula na pia kutupeleka katika maeneo tulimokuwa na miadi za kukutana na tuliowakusudia. Katika baadhi ya nchi, walikuwepo waliojitolea kutuchukulia hoteli ili tupate utulivu zaidi wa kufanya kazi zetu.
 
Kwa wale wengi waliokuwa wakistaajabu vipi tukiweza kufanikisha ziara kubwa na refu kama hizi, basi hii ilikuwa ndiyo siri yake. Tuyawache hayo kwa sasa.

Moja ambalo lilikuwa ni jambo la desturi kwa Maalim Seif mnapofanya ziara kama hizi na ikiwa mmefuatana naye lilikuwa ni kuhimiza kufika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi husika kwa ajili ya kusalimiana na Balozi na maofisa wake. Nakumbuka tulifanya hivyo takriban kila nchi tuliyokwenda ambayo Tanzania ina Ubalozi.
 
Ikiwa ni sehemu ya ratiba yetu tukiwa nchini Marekani, tulifika jijini New York mwezi Februari 2004 tukiwa tumekwenda kwa lengo la kufika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na kukutana na Msaidizi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa a ayeshughulika na Mambo ya Siasa. Pia tulikuwa na ratiba ya kwenda Taasisi ya International Peace Academy (sasa inaitwa International Peace Institute) ambayo Ofisi zake haziko mbali na Umoja wa Mataifa na hapo tulikuwa na miadi ya kuonana na Mkurugenzi wake anayeshughulikia masuala ya Afrika.
 
Basi baada ya kumaliza mikutano hiyo, tukiwa tunatembea kwa miguu, Maalim Seif akanambia twende Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa tukawasalimie. Hatukuwa na miadi. Maalim akanambia twende tu. Tuliiona Ofisi kabla wakati tunaelekea Makao Makuu ya UN.

Tukatembea taratibu maana hatukuwa na haraka. Tukafika katika jengo lililokuwa na Ofisi nyingi ikiwemo ya Ubalozi wa Tanzania. Tulipofika tukaelekezwa ghorofa ulipo Ubalozi huo.
 
Tulipofika tukagonga mlango na tukafunguliwa na mtu wa mapokezi. Maalim Seif hakuhitaji kujitambulisha. Sura yake hakuna asiyeitambua sikwambii kwa watumishi wa Ubalozi wa Tanzania. Basi Maalim akamwambia mtu wa mapokezi kwamba tumekuja kumsalimia Balozi kama yupo. Hakungoja aulizwe, akamwambia hatuna miadi. Tukakaribishwa tukae na tukaambiwa tusubiri.
 
Haikuchukua hata dakika tano, tukamuona Balozi anakuja kutufuata (bila ya shaka kwa heshima ya Maalim Seif). Balozi huyo alikuwa ni Dr Augustine Mahiga. Mimi sikuwa namjua kwa sura kabla ya hapo lakini nilishamsoma na kumsikia sana habari zake hasa kuhusiana na wakati wake akiwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa wakati wa jaribio la kuipindua Serikali ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1983.
 
Kama kawaida yake alikuwa kavalia vizuri ikiwa ni moja ya alama za mwanadiplomasia anayejitambua. Kwenye shughuli za itifaki, kuonekana vyema (mtanashati) ni moja ya kipimo cha kuielewa hadhi na haiba ya kazi hiyo.

Alipotujia tu na jinsi alivyotusalimia basi niliona dalili za mtu muungwana. Akizungumza kwa heshima kubwa mbele ya Maalim Seif pamoja na kuwa hawakupishana sana kiumri. Maalim alinitambulisha kwake lakini mimi niliamua kuwaachia wakubwa wenyewe wazungumze. Nikabaki kuwa msikilizaji na nikaomba ruhusa ya Balozi kuwapiga picha ambayo ndiyo hii niliyoiambatanisha hapa.
 
Maalim Seif alimtaka radhi kwamba tumemshtukiza na kwamba hatukuwa na miadi. Balozi Mahiga kwa uungwana kabisa akamjibu Maalim kuwa Ubalozi ni nyumbani kwa kila Mtanzania na mtu hahitaji miadi kwenda nyumbani kwao. Maalim akamshukuru kwa wema na ukarimu wake.

Katika mazungumzo yao ndipo nilipobaini siyo tu uweledi wa Balozi Mahiga katika kazi ya Usalama ambayo alitokea lakini pia jinsi alivyokuwa mahiri wa fani ya diplomasia aliyokuwa anaifanyia kazi. Bila ya shaka alijaribu kutaka kujua kilichotuleta UN na pia kama tumeonana au tutaonana na watu wengine nje ya UN. Na Maalim kama kawaida yake na akitumia uzoefu wake hakutaka kutoa nafasi ya kuingia undani wa hayo.
 
Lakini pamoja na hayo, Balozi Mahiga alimuuliza Maalim kuhusu hali ya kisiasa ilivyokuwa Zanzibar na maendeleo ya Muafaka wa Pili ambao wakati huo ulikuwa unaendelea na utekelezaji wake. Katika hilo Maalim alimueleza kwa kina hali ilivyokuwa na akamwambia kuwa mtihani mkubwa utakuwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliofuata ambao ulikuwa ni wa mwaka 2005. Balozi Mahiga akamwambia Maalim Seif kwamba wao walioko katika Ofisi za Ubalozi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchi za nje huwa wanapata wakati mgumu sana kujibu maswali yanayohusu hali ya kisiasa Zanzibar na hivyo wanapendelea sana mambo yende vizuri.
 
Basi baada ya mazungumzo hayo, tuliagana naye na yeye akaendelea kuonesha tabia yake ya kiungwana kwa kutusindikiza hadi kwenye lifti.

Kwa hakika, kama wengi wanavyoeleza tokea taarifa za kifo chake zilivyotangazwa jana asubuhi, Balozi Augustine Mahiga alikuwa na khulka tofauti sana na zile za kiburi na majivuno ya utawala ambazo zimezoeleka kutoka kwa viongozi wengine wa CCM. Si ajabu basi kuona hata viongozi wa juu wa vyama vya upinzani wakimsifia na kumlilia.
 
kwetu sisi msiba unaisha baada ya siku 40
vumilieni bwanaaa

================

Maalim Seif Sharif Hamad wakati huo akiwa Waziri Kiongozi wa #Zanzibar akizungumza katika dhifa ya taifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake wakati alipofanya ziara rasmi ya kiserikali nchini #Singapore mwaka 1987.

Dira ya kuifanya Zanzibar kuwa Singapore ya Afrika Mashariki haikuzuka tu!
1615745304807.png
 
DOWN MEMORY LANE:
Contributed by #Zanzibar to Britain during First World War 1914 - 1918. Photo Courtesy: Zanzibar National Archives.

KUMBUKUMBU:
Ndege hii ya kivita ilinunuliwa na Zanzibar na kutolewa msaada kwa Uingereza wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia 1914 - 1918. Picha kwa hisani ya Idara ya Nyaraka, Zanzibar.
1615745408730.png


Tanganyika mulishawahi kuwa dona countryyyyyyy.?
sisi tuliwahi kuwa urojo countryyyyyy
 
Back
Top Bottom