Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1615956782081.jpg
 
Demokrasia, haki na uhuru. Ni dhana tata ajabu. Japo kila mtu ana haki na uhuru wa kutenda anachotaka lakini pia ni lazima kuangalia matakwa ya wengi. Na hapo ndipo dhana ya demokrasia inaingia. Kwamba uhuru wako wa peke yako kutaka kufanya ukitakacho unaweza kuzimwa na uhuru wa wengi kama kitu unachotaka kukifanya hakiwapendezi wengi. Na huu ni msingi wa muhimu sana katika kuleta utangamano katika jamii vinginevyo kila mtu angekuwa anafanya tu anachotaka akidai kuwa ni uhuru wake haijalishi kama analolifanya linawakera wanajamii wenzake.

Na huwezi kuwa mpigania demokrasia, haki na uhuru (wa kweli) kama huheshimu maoni ya wengine - hasa ya walio wengi kwa sababu huo hasa ndiyo msingi wa demokrasia unayoipigania. Kwamba wewe ndiyo wewe, ulitakalo lazima lifanyike kwa sababu ni haki yako; na uhuru wako uko juu ya kila mtu. Hapana! Huu ni udikteta!

Tumeishi katika uzi huu kwa amani na upendo sana kwa sababu kuna misingi ambayo tulikuwa tumejiwekea. Misingi ambayo ilituepusha na chuki na ugomvi - kuepuka siasa, dini, matusi na picha za utupu. Kwa kufuata misingi hii tumejenga urafiki na undugu humu. Inaumiza kuona kuwa leo hii tunatukanana sisi kwa sisi. Ndiyo maana wengine hatuonekani sana katika uzi huu tena.

Jukwaa la siasa lipo. Jukwaa la dini lipo. Anayeyataka haya ayafuate huko na akaporomoshe matusi yake huko; apate na ban yake huko. Mtuachie kijiwe chetu hiki cha upendo tuendelee kucheka na kufurahi. Vinginevyo bakini na uzi wenu !!!

Demokrasia. Haki. Uhuru !!!
Amun Ra
 
Back
Top Bottom