Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwaka 1915, mwanamke mmoja alichelewa kwenye mazishi ya dada yake aliyeitwa Essie Dunbar aliyekufa akiwa na miaka 30. Alipofika, aliomba jeneza la dada yake lifunguliwe ili aweze kumuona kwa mara ya mwisho. Baada ya kufungua jeneza, yule mwanamke aliyekufa (Essie) alinyanyuka na kutabasamu. Aliishi kwa miaka mingine 47 ndipo akafa.
 
Mwaka 1915, mwanamke mmoja alichelewa kwenye mazishi ya dada yake aliyeitwa Essie Dunbar aliyekufa akiwa na miaka 30. Alipofika, aliomba jeneza la dada yake lifunguliwe ili aweze kumuona kwa mara ya mwisho. Baada ya kufungua jeneza, yule mwanamke aliyekufa (Essie) alinyanyuka na kutabasamu. Aliishi kwa miaka mingine 47 ndipo akafa.
 
Kama unaona unachelewa sana kusubiri hadi ufikishe miaka 18 ndo uruhusiwe kunywa pombe kisheria Tanzania, basi wewe usingeweza kuishi Aztec. Karne ya 13 katika bara la Amerika ya kaskazini kulikua na Himaya/Ufalme ulioitwa Aztec (Aztec empire). Katika Ufalme huo umri wa mtu aliyekua anaruhusiwa kunywa pombe ni kuanzia miaka 70 na kundelea tu. Miaka 69 kushuka chini walikua hawaruhusiwi kunywa pombe.
 
Mwaka 1996, Jim Kardach alipendekeza jina Bluetooth litumike kama jina la teknolojia iliyoundwa ili kusaidia uhusiano na ushirikiano wa kuunganisha na kubadilishana data kutoka katika vifaa viwili (Two devices). Kardach alinukuliwa akisema, "Mfalme Harald Bluetooth ... alikuwa maarufu kwa kuunganisha Scandinavia kama vile tulivyokusudia kuunganisha vifaa bila kutumia waya." Jina Bluetooth lilianzia zaidi ya miaka 1000 iliyopita (millennium) kwa Mfalme Harald "Bluetooth" Gormsson ambaye alikuwa anajulikana sana kwa vitu viwili: Kitu cha kwanza ni Kuunganisha Denmark na Norway mnamo mwaka 958. Pili ni jino lake lililokufa, ambalo lilikuwa na rangi ya bluu na likampatia jina la utani Bluetooth.
 
Mwanaume mmoja kwa jina la Ma Van Nhat raia wa Vietnam, mwaka 2017 alienda hospital baada ya kusumbuliwa na tumbo muda mrefu. Baada ya kufanyiwa vipimo aligundulika ana mkasi tumboni ambao ulisahaulika alipokuwa amefanyiwa upasuaji. Upasuaji huu ulifanyika baada ya kupata ajali ya gari mwaka 1998 na bila Kujua wakasahau mkasi tumboni. Mkasi huo ulikuja kugundulika na kutolewa miaka 18 baadaye, mwaka 2017 siku alipoenda hospitali. Mkasi ulikutwa ukiwa na kutu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…