Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Msanii Juma Kilaza (mwenye alama nyekundu) alijifanya anajua kupiga gitaa kuliko Mbaraka mwinshehe miaka ya 1970, lakini Siku waliposhindanishwa akaonekana kuwa na uwezo mdogo sana. Tangu hapo watu wenye uwezo mdogo kufanya mambo huitwa "vilaza". Yakiwemo masomo ya darasani.
 
Miaka ya 1900 Kulizuka Wanywa Damu za Watu, Mavampire Lousiana US, Mmoja Kati ya Mavampire Hao Alikuwa ni Mbishi Auguste Delagrange Aliyewauwa na Kuwanyonya Damu Zaidi ya Watu 40, Alikuwa Mgumu Kufa, Alipokufa Alitolewa Moyo na Mifupa Yote kwa Maonyesho
 
Wanawake wengi wenye mvuto mara nyingi hawapo kwenye mahusiano. Hii ni kwa sababu wanaume wengi hufikiri wanawake hawa wana wapenzi tayari hivyo huogopa kueleza hisia zao. Fungukeni wazee
 
Martin Laurello kutoka Ujerumani ndiye mwanadamu pekee aliyekuwa na maajabu kwenye kichwa chake kiasi cha kuwaacha wanasayansi vinywa wazi.

Martin alikuwa na uwezo wa kugeuza kichwa chake kwa nyuzi 180 na kuangalia kitu cha nyuma yake bila kugeuza mwili. "Human Owl".
 
Umewahi kujikuta ukiongea mwenyewe kichwani kiingereza unakijua ila ukisema ufungue mdomo sasa kigugumizi kinaanza?Hii ni kwa sababu akili yako inajua namna ya kutamka maneno hayo lakini ulimi haujui. Unahitaji mazoezi zaidi ya ulimi ili kuzoea.
 
BRUCE LEE alikua sio tu muigizaji bali pia mkufunzi wa daraja la juu wa mchezo wa "Martial Arts"; inasemekana pia ni mwanzilishi wa baadhi ya FALSAFA za mchezo huo ambazo zimefanya mageuzi makubwa na zimekuwa nguzo muhimu za mapigano duniani kote
 
KUTAHIRIWA👇

Je unajua kuwa watu wa Kwanza kuanzisha utaratibu wa kutahiri ni waafrika??Ndio mpaka sasa hivi kwa mujibu wa tafiti ni kuwa taifa la Misri ndio taifa la kwanza kuanzisha utaratibu wa kutahiri wanaume

Wanasayansi wamegundua mchoro wa Uume uliotahiriwa
 
Jean Lafitte, Alikuwa Haramia na Mtekaji Meli Mkubwa Raia wa Ufaransa Karne ya 18. Kuna Kiongozi Mmoja wa Serikali Alitangaza Dau la $500 kwa Atakayefanikisha Kukamatwa kwa Jean. Jean Naye Akatoa Dau la $5,000 kwa Atakayefanikisha Kiongozi Huyo Kutekwa
 
MIZINGA 21

21 Tank/Gun Salute.

Umekua utamaduni wa KIJESHI Kwa KARNE 7 sasa. Mwanzoni ulikua ukitumika na VIKOSI vya wana maji barani ULAYA kama ishara ya AMANI. Baadae ukabadilishwa na kuwa ISHARA ya HESHIMA. Kutoka ULAYA hadi AMERIKA na sasa DUNIANI kote.
 
James Buchanan, Rais wa 15 wa Marekani aliyekalia kiti cha Urais mnamo mwaka 1857 hadi 1861.Huyu ndiye Rais pekee wa Marekani ambaye maisha yake yote hakuwahi kuoa wala kuishi na mwanamke.
 
Mwana Mama Dr Jane Goodall,Mbobezi, nguli, mashuhuri, mwana mazingira na mtafiti na mtetezi wa wanyama na mazingira. Dr Jane anafahamika kwa utafiti wa sokwe aliofanya kwa miaka 26 katika hifadhi ya Gombe Kigoma Tanzania. Msukumo mkubwa katika kutimiza lengo lake
 
Kusuka nywele ni ustaarabu wa muafrika tangu enzi na enzi,misuko ilibeba maana na tafsiri kubwa sana kama vile ukoo,utajiri pia hata njia ya mawasiliano ya kijasusi n.k
 
Kupata ndoto mbaya (jinamizi) mara kwa mara kunaweza kusababisha wasiwasi mwingi, sonona (depression) na matatizo mengine. Anayepata ndoto mara kwa mara inakuwa ni sababu ya kuwa na siku yenye mahangaiko & anahitaji kufanya mabadiliko haraka
 
Isaack Newton aliwahi kua mbunge wa bunge la england hakuwahi kuchangia chochote ,baadhi ya wanahistoria wanasema aliwahi kulalamika kuhusu hali ya hewa ndani ya chumba cha bunge akiomba dirisha kufinguliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…