Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1616789747900.jpg
 
Martin Laurello kutoka Ujerumani ndiye mwanadamu pekee aliyekuwa na maajabu kwenye kichwa chake kiasi cha kuwaacha wanasayansi vinywa wazi.

Martin alikuwa na uwezo wa kugeuza kichwa chake kwa nyuzi 180 na kuangalia kitu cha nyuma yake bila kugeuza mwili. "Human Owl".
 
Ulaji wa bamia mara kwa mara kwa wanawake husaidia kuponya kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi mara kwa mara na hutibu pumu. Kwa wanaoitumia mara kwa mara, huongeza kinga ya mwili.
 
Miaka 1970s mpaka 1980s biashara ya madawa ya kulevya ilianza kushamiri kwa kasi nchini Mexico,Genge maarufu la Guadalajara liliongozwa na Kingpin Miguel Felix Gallardo(El Padrino), awali walisambaza zaidi Marijuana kabla ya kujikita zaidi kwenye biashara ya cocaine
 
Mwanafizikia Max Planks alishauriwa na Profesa aliyekuwa mwalimu wake kwamba asiingie kwenye "field" ya fizikia kwa sababu karibu kila kitu kimeshavumbulia. Licha ya ushauri, Max aliingia na mwisho wa siku alivumbua "Quantum Theory" ambayo ilibadili kabisa fizikia
 
Mwaka 2013, Serikali ya Korea Kaskazini ilianzisha sheria ambayo inawapa mamlaka ya kuwachagulia raia wake mitindo (styles) ya nywele

Mitindo 18 kwa wanawake na 10 kwa wanaume. Katika mitindo yote, Mtindo wa Rais Kim Jong-un haukujumuishwa kwenye orodha iliyotolewa
 
Chokoleti (Chocolate) ina kiwango kikubwa cha kemikali aina ya Theobromine & Phenylethylamine ambazo husaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi.
 
Ghuba ya Alaska ndio sehemu pekee ya makutano ya bahari kubwa za Pasifiki na Antlantiki. Kinachoshangaza ni kuwa maji ya bahari hizo hayajawahi kuchanganyika

Kila upande hubaki na maji yake. Sababu nyingi zinatajwa kama vyanzo vya ajabu hilo ingawa hazina uthibitisho
 
Mwaka 2018, kampuni ya magari ya Mercedes-Benz katika kutangaza umadhubuti na nguvu ya taa za gari zao. Walitumia picha inayoonesha MWANGA wa taa za gari hilo ukipenya ndani ya mwili wa ng'ombe. Picha hii ilisifiwa kwa ubunifu mkubwa uliotumika.
 
Unajua Tinker Toy ndiye PAKA mdogo kuliko wote kwenye historia ya dunia. Mwaka 1997 akiwa na miaka 7 wakati anakufa alikuwa na urefu wa 7cm (2.75 inch) kutoka kichwani hadi miguuni na 19cm (7.5 inch) kutoka kichwani mpaka kwenye mkia. Mdogo kuliko PANYA wa kawaida wa nyumbani
 
Kwa mujibu wa watafiti kukumbatiana (cuddling) kabla ya kulala husaidia kumpa mtu amani ya moyo na akili hivyo kumpunguzia mkazo (stress) na kumfanya apate usingizi haraka.
 
Saikolojia inasema kukosa usingizi ama kukaa na njaa kwa muda mrefu ni sababu kuu mbili zinazopelekea mtu awe na hasira zisizo na msingi wowote. Pata usingizi wa kutosha pia kula kila inapobidi ili uache kutisha na kukasirikia watu hovyo
 
Lamba kiwiko cha mkono wako, subiri sekunde 5 hadi 10, kisha nusa kiwiko hicho. Harufu utayoiskia ndo watu wanayoiskia kutoka mdomoni mwako

Da'Vinci
 
Hii ni muhimu zaidi kwa wanafunzi hasa wagumu wa kushika kichwani vitu wanavyosoma. Kusoma kitu kwa sauti kuonaongeza uwezekano wa kukikumbuka maradufu zaidi ya kukisoma kimyakimya
 
hata uwe na hasira kiasi gani, hata uwe na majonzi kiasi gani, kitendo cha kutabasamu kidogo tu kitakupa ahueni kwa sababu kutabasamu hushtua mishipa "inayotekenya" kemikali za furaha ubongoni
 
Mwamba Placido Galindo wa Peru ndio binadamu mwenye rekodi ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya kwanza kwenye kombe la dunia,alitolewa uwanjani dakika ya 54 ya mechi kati ya Peru na Romania kwenye world.cup.ya 1930
 
Wanawake wengi wenye mvuto mara nyingi hawapo kwenye mahusiano. Hii ni kwa sababu wanaume wengi hufikiri wanawake hawa wana wapenzi tayari hivyo huogopa kueleza hisia zao. Fungukeni wazee
 
Back
Top Bottom