Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Akifuata nyayo za jiwe dhuluma na udhalimu ni lazima akomaliwe na Watanzania wote si BAVICHA tu Mkuu wale wenye mapenzi ya kweli na Nchi yetu. Jiwe limeumiza Watanzania wengi sana wadogo kwa wakubwa, limefuja sana pesa za walipa kodi in trillions na limeiacha Nchi mahali pabaya sana.
Aaaah nyie BAVICHA hamna mema kabisa 🀣 🀣 🀣🀣
Muda si mrefu mtaanza kumrushia mawe mama wa watu!
 
Muangalie MNAFIKI mwingine huyu Mkuu.
View attachment 1737235
Hahahaha mkuu BAK hawa vijana wanafiki na walevi wa madaraka mbona tunawafahamu vizuri sana tu!!
Lakini sisi tunachotegemea kutoka kwenu BAVICHA ni kwamba tujitahidi kuweka pembeni siasa za vyama!
Nchi yetu sote hii mazee, kumbuka jinsi ambavyo CHADEMA walimtukana Mzee Kikwete lakini wakamkumbuka.

NB: Sasa kwenye ukweli, tuseme ukweli tusifanye uzandiki wala kupiga propaganda za kitoto, nchi changa hii! Pia kama CCM hawajajifunza kuacha unafiki na kuheshimu katika kipindi hiki basi hawawezi kujifunza tena.
 
Hakika, asipoheshimu Katiba ni lazima ashughulikiwe tu, hakuna namna. Lakini kwasababu taifa letu bado lina majeraha na mpasuko mkubwa, na Raisi kaonesha nia njema kabisa ya kutaka kutibu hayo madonda ndugu, basi tumpe muda na kumuunga mkono. Panapohitajika kukosoa tukosoe lakini tusifanye uzandiki na hujuma zisizo na kichwa wala miguu.

NB: Mimi nakumbuka Mzee wangu Mbowe aliwahi sema, Tanzania inahitaji Dikteta kwasababu Kikwete ni Laissez-Faire , sasa walipopata Dikteta waliyemtaka wakaanza tena kulalama. Nadhani siasa za namna ile ni za kuchumia tumbo na hazitakiwi kupewa nafasi tena hapa nchini. SIASA MAJI-TAKA na MATUKIO.
 
Kama nchi ni yetu sote basi tukemee maovu yote na dhuluma bila kukwepesha na kusifia UPUMBAVU huku Nchi ikizidi kwenda alijojo na kuonekana kituko duniani.
 
Sentensi ya mwisho umemaliza kila kitu[emoji122]
 
Kama nchi ni yetu sote basi tukemee maovu yote na dhuluma bila kukwepesha na kusifia UPUMBAVU huku Nchi ikizidi kwenda alijojo na kuonekana kituko duniani.
Off-Course, hii ndiyo kasumba ambayo imewakumba wasomi wengi wa nchini Tanzania: Wako radhi wauze uhuru wao kwa wanasiasa wakiamini watapata maendeleo ya haraka. Nadhani walioamua kuweka Bill of Rights kwenye Katiba mwaka 1984 na kuruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 hawakukosea na waliona mbali sana. Watanzania wengi tulisahau haya na kuanza kuunga mkono hata mambo ambayo hayana msingi tukiamini kwamba ni uzalendo.

Binafsi, kuna mambo ambayo mzee Magufuli ameyafanya ambayo ni makubwa sana kwa nchi hii na siyo sawa kuyasema hadharani. Mkuu BAK kule kwenye madini kulikuwa kumeoza sana mazee, yaani kumeoza mno. Watu walikuwa hadi na mipango ya kuanza kuchimba Uranium kinyemela lakini mzee Magufuli akapiga rungu kubwa sana: Kipindi kile cha Ripoti za MAKINIKIA, CHADEMA wakiongozwa na LISSU walifanya UZANDIKI na HUJUMA za waziwazi dhidi ya Tanzania bila kufahamu kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia.

Alichokosea na kilichomponza huyu mzee ni tabia yake ya kuvunja Katiba: Hasahasa kuminya uhuru wa watu, uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu (mauaji, utekaji na utesaji), kuingilia mahakama, matumizi makubwa ya fedha bila idhini ya bunge (akiamini ndiyo Ujamaa), ushughulikiaji mbovu wa Covid-19 na kuvuruga kabisa diplomasia ya nchi.

Mengine aliyotufanyia tunasamehe kama binadamu, maana kama kuumia tuliumia wengi hivyo siwezi kuanza lalamika hapa. Vivyo lazima tukubali kwamba kuna mema mengi aliyafanya pia: Nadhani kukubali huu ukweli ni jambo la kiungwana.
 
πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½
 
Huko kwenye madini ni UOZO MTUPU Mkuu ila ngoja ninyamaze tu. Wizi na ufisadi kila kona Mkuu huku tukifanyiwa viini macho eti alikuwa ANAINYOOSHA Nchi!!!
 
BAK hajui kuappreciate kitu hata kama kina ukweli.

Siasa za majitaka...wao kila kitu ni kupinga tu..hovyoo !
 
😳😳😳😳😳😳😳
Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu narudia tena ngoja tu ninyamaze kuhusu UOZO kule kwenye madini. Tulikuwa tunaibiwa sana na kwenda kufichwa nchi ya jirani 🀐 Jiwe ni dhalimu na dhulmat mkubwa sana kaitendea maovu mengi sana nchi hii tangu awamu ya tatu. Watu wengi tulijua jiwe ni bomu na janga kubwa la Taifa hata kabla ya kuwa nominated kama mgombea wa ccm na kile tulichokidhania tangu July 2015 kaika hii miaka mitano na ushee kimekuwa ni ukweli mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…