Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mama kwa kweli kaanza kwa gia kubwa sana. I hope atabaki hivi.Akiheshimu raia, katiba, Bunge, mahakama, kuongoza kwa haki na uwazi kutuletea katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi basi anaweza kabisa kujizolea sifa nyingi sana si ndani ya Nchi tu bali hata nje ya mipaka yetu.
Kabisa.. asisikilize wafia chama
 
Screenshot(23).png
 
Katika hili Mzee wangu Magufuli hakushauriwa vizuri ndiyo maana alipoteza pesa nyingi sana. Ukisoma Sheria za Usafirishaji wa anga, mara nyingi mataifa mbalimbali hayanunui kabisa ndege bali huwa yanakodi (Aircraft-Leasing) ili kukwepa gharama. Lakini sasa ukinunua kwa fedha taslimu gharama inakuwa kubwa zaidi kwasababu, unaanza kutengenezewa ndege mpya: Hapa sasa inabidi uanze kulipia chumba (Slot) ambapo ndege hiyo mpya itatengenezewa.

Makosa mengine ya mzee ni kuwaachia hii mikataba mikubwa ya manunuzi ya ndege isainiwe na wanasheria wa Ubalozi ambapo wengi wao Aviation Law & International Law hawajasoma. Lakini makosa makubwa ni kuimilikisha serikali ndege wakati tuna madeni makubwa ya kimataifa ambayo tunadaiwa na makampuni na watu binafsi: Unakumbuka Bombardier zilivyokamatwa Canada na S.A ??? Tulitumia gharama nyingi sana kwenda kuzitoa kwasababu ya Pomposity ilhali tungeweza kukwepa ndege kukamatwa.

Mfano tungeweza hata kusema zile ndege ni mali za Ubalozi na zinatumika kwa shughuli za kibalozi hivyo zingepewa Immunity kama Consular Properties na kulinda chini ya Vienna Convention on Consular Properties. Hivyo ATCL ingetengeneza mkataba na ubalozi ili ikodi zile ndege, AU tungesajili kampuni lolote nchini Uchina ambako ni Marafiki wa Tanzania na kampuni likaoneka ni la Uchina na limetuazimisha (Aircraft Leasing) sisi Tanzania. Lakini sasa mzee alikuwa anasema anataka dunia ijue kwamba sisi tumenunua ndege kwa fedha zetu.

Halafu utakwambia ninyi, wanasheria ni waoga waoga sana 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
Daaah Rest in Peace Mzee Magu, your intentions were pure but tactics very questionable.
 
Mama kwa kweli kaanza kwa gia kubwa sana. I hope atabaki hivi.Akiheshimu raia, katiba, Bunge, mahakama, kuongoza kwa haki na uwazi kutuletea katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi basi anaweza kabisa kujizolea sifa nyingi sana si ndani ya Nchi tu bali hata nje ya mipaka yetu.
Aaaah nyie BAVICHA hamna mema kabisa 🤣 🤣 🤣🤣
Muda si mrefu mtaanza kumrushia mawe mama wa watu!
 
Ndiyo shida ya mtu mweusi hii duniani kote. Ubinafsi. Ujinga. Kutojali. Rushwa isiyojali. ...Ndiyo maana hata tukitupiwa maganda ya ndizi huko mi sishangaagi sana. Ndiyo ufisadi upo kila nchi lakini huu wa kwetu huku Afrika bado unaakisi ujima wetu na pengine hata unyama wetu. Haiwezekani uibe $50 millions zilizopangwa kujengea vituo vya afya 100 vijijini halafu ubakie kuwa na furaha we na familia yako kuwa mko wajanja na mmetajirika huku watu uliowaibia wakifa kwa kukosa aspirin. Hata nafsi haikusuti? Ubinadamu wako uko wapi?
Kwakweli inaumiza sana sijui waafrika tuna shida gani. Yaani mtu unakuaje na roho hii? Unazaliwa nayo au inakujia tu?? Nyie mliotembea tembea na wenzetu huko hawajali maisha ya wengine??
Sometimes bora kutozaliwa tu kwakweli..
Kuhusu kutaifisha mali za mafisadi hawa ni tatizo la kimfumo zaidi. Ni vigumu sana kuthibitisha mahakamani kuwa yupi na yupi ndiye kaiba na hata ukithibitisha bado kuna miongozo ya kisheria itakayokubana. Usipoifuata utaitwa dikteta. Na kwa vile ufisadi huu unagusa kila sekta mpaka madini, utajikuta unapambana na cartels za kimataifa. Ukizubaa wewe ndo utakufa na kuyaacha mafisadi yakidunda. Usifikiri kuwa marais wote hawa Afrika hawana uzalendo. Wengine wazalendo kweli lakini wakiingia tu madarakani wanakuta mfumo unatisha na wanasarenda.
Daah yaani unafaidika Vipi kukusanya mali ambazo muda wote utaziacha?? Tena kwa njia haramu?? Kweli maisha ni fumbo
Hata tukikupa leo wewe uwe rais utapambana na mifumo hasimu sana na ukivimbisha kichwa utauliwa tu. Kama unabisha kamuulize JPM atakuambia !!!
Aisee naona unanizidishia majonzi..Mungu amrehemu tu raisi wetu. Ametuomyesha rangi ya wanadamu walivyo
 
Back
Top Bottom