Unajua shida kubwa ni kwamba mzee alizungukwa na wapiga vigelegele wengi ofisini kwake, huku mitandaoni na duniani. Wengi ya wasaidizi wake walikuwa wanalinda ugali wao hivyo walimwambia mambo ambayo yeye alitaka kuyasikia. Watu kama wakina Lawrence Mafuru (Former Treasury Registrar) na uwezo wao wote, walipomwambia ukweli kuhusu uchumi na matumizi ya pesa walifukuzwa hazina.
Nakumbuka Lawrence alimwambia mzee kwamba, anavyobomoa Uchumi akisema ananyoosha mafisadi, uchumi hauwezi kurudi juu ndani ya miaka miwili ya mwanzo. Eeeh mzee akamfukuza kule hazina, lakini Lawrence alipohojiwa Clouds nakumbuka akarudia kusema wazi kabisa kwamba Uchumi wa nchi hauwezi kurudi juu leo wala kesho. Wapiga vigelegele walimbeza sana, lakini leo hii yako wapi ???
Kuna vitu kama Raisi angeambiwa mapema na washauri wake bila kuogopwa, nadhani asingekosea sana kwenye Uchumi maana asingeshindana na watu wote. Lakini shida inakuja pale ambapo watanzania wengi ni watu wanaopenda unafiki na kupenda kusifia mambo hata kama hayana tija kwa taifa, wakiamini ndiyo uzalendo. It's just lackadaisical.....