Lakini, shida itakuwa sehemu moja tu, mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy hatakuwa tayari kumpoteza mchezaji huyo, hivyo atamuuza pesa nyingi, haipungui Pauni 150 milioni na hilo ndilo litakalomfanya asiondoke, kwa sababu kwa hali ya sasa hakuna klabu itakayokuwa na jeuri ya kulipa pesa nyingi hivyo kusajili mchezaji mmoja.