Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 183,580
- 1,105,911
Pole sana mkuu. We endelea tu kupambana. You never know...Nina majonzi hapa mkuu, muhusika hajawahi kujibu mpaka hivi tunavyoongea, alinitoa kwenye ignore list ila PM yake imefungwa kabisaa, nimejaribu mara kadhaa lakini amefunga, kikichonistua leo nimejaribu kumchungulia naona ana bango la banned, napata mashaka nahisi labda ameamua kuwaomba mods wafunge accout yake moja kwa moja maana nimefuatilia posts zake za miezi miwili iliyopita sijaona kama ameandika jambo lolote linalopelekea yeye kuwa banned,nimejikuta nawaza sana halafu nakosa raha
Au pengine ule uzi ukimkasirisha kiasi kwamba ameamua kuondoka JF moja kwa moja?
Kama ni ban pengine yatakuwa ni haya mambo ya siasa kwa kuwa huwa hatukani na hana lugha ya ukakasi wala malumbano ya kijinga. Si shabiki sana wa marehemu na pengine kuna mahali kasema kitu mods wakapita naye...