Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BARAKOA ZA PUA ZIMEKUJA _ Watafiti nchini Mexico wanadai kuwa wamebuni mtindo mpya wa Barakoa (mask) ambao utamuwezesha mtumiaji kuweza kula, kunywa na hata kuzungumza huku akiwa bado amejilinda dhidi ya Virusi vya Corona. Barakoa hiyo ambayo imezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii na kuitwa 'maski za pua' zilionekana kuvaliwa na mwanaume mmoja na mwanamke ambao majina yao hayakuweza kutambuliwa wakiwa wamekaa katika mgahawa wakipata chakula. Kipande cha video ambacho kilisambaa kupitia shirika la habari la Reuters walionekana wawili hao wakivua Barakoa zilizoziba mdomo na ndani yake kukiwa na hizo ambazo si zakawaida huku wakipata chakula wakiwa pamoja.
 
Muda mwingine sayari ya Venus wanaiita dada yake dunia sababu ina ukubwa na uzito unaokaribiana na sayari yetu ya dunia, pia wananaiita hivyo sababu umbali wake hadi kwenye jua huatofautiani sana na umbali toka duniani hadi kwenye jua.... sasa usije kusikia kua Venus ni dada yake dunia na wewe ukapanga safari ya kwenda huko,, Yani utaona moto..
 
Kwanza sayari ya Venus ndio sayari yenye joto zaidi ya sayari nyingine yoyote kwenye mfumo wetu wa jua, Joto lake linafikia mpaka 464°C... sasa joto hili linaweza kukuchoma kama mishikaki, maana kumbuka maji yanachemka kwa nyuzi joto 100°C tu, pia kumbuka chuma kinachofahamika kwa jina 'Lead' kinayeyuka kwa 300°C tu... fikiria sasa joto hili litaufanyaje mwili wako wewe.
 
Hewa inayopatikana katika sayari ya Venus ni 96%Carbon dioxide,, pia mvua inayonyesha ni mvua ya Sulfuric acid, hii acid ni hatari sana,
kama unaijua nadhani utakua unanielewa maana kwanza inaweza kukutoboa ngozi, macho, pua na kila kitu na inanuka zaidi ya yai viza.
 
Atmospheric pressure katika sayari ya Venus 93 bar,, yani ukiwa katika sayari hii, pressure utakayoisikia ni sawa na jinsi unavyojisikia ukiwa chini kabisa ya bahari, kwa pressure kama hii ukijaribu kukanyaga mguu wako katika sayari ya venus, mwili wako utavunjwa vipande vipande ndio maana hata jiwe lolote kubwa(Asteroid) likijaribu kutua katika sayari ya Venus litavunjwa vunjwa vipande kabla hata halijatua..
 
Je wajua pia sayari ya venus ndio sayari ya kwanza mwanadamu kutuma chombo chake cha anga huko, na hii ilikua mwaka 1962 ambapo chombo kilichotumwa kiitwacho Mariner 2 kilipoteza mawasiliano lakini chombo kingine Venera 7 mwaka 1970 kiliweza kutua katika Ardhi ya Venus ila hakikupoteza muda maana kilivunjwa vunjwa vipande,, vipo vyombo vingine pia vilivyowahi kutumwa ila vilivunjwa vunjwa na pressure iliopo katika sayari ya Venus ndio maana mda mwingine sayari hii inaitwa Spacecraft Breaker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…