Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baba yake Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, Alf-Inge, na ajenti wake Mino Raiola watakuwa na mikutano London na Manchester City, Chelsea, Manchester United na Liverpool Ijumaa juu ya uhamisho wa mchezaji huyo, 20, raia wa Norway. Tayari wawili hao wamefanya mazungumzo na Barcelona na Real Madrid. (Mundo Deportivo - in Spanish)
 
Kiungo wa kati wa Arsenal raia wa Uruguay Lucas Torreira, 25, ambaye yuko kwa mkopo Atletico Madrid, amesema kuwa anataka kurejea Amerika Kusini baada ya kutokea kwa kifo cha mama yake na sasa hivi amelenga kujiunga na klabu ya Argentina Boca Juniors kutimiza ahadi aliyoweka kwa baba yake. (ESPN Argentina, via Goal)
 
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema hatma ya mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette itajadiliwa msimu huu, wakati ambapo mchezaji huyo, 29, anahusishwa na Roma, Atletico Madrid na Sevilla - atakuwa amesalia na miezi 12 katika mkataba wake wa sasa. (Guardian)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…