Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baba yake Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, Alf-Inge, na ajenti wake Mino Raiola watakuwa na mikutano London na Manchester City, Chelsea, Manchester United na Liverpool Ijumaa juu ya uhamisho wa mchezaji huyo, 20, raia wa Norway. Tayari wawili hao wamefanya mazungumzo na Barcelona na Real Madrid. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Duuu, wako vizuri.
Hawataki janja janja, unaitwa, unasikilizwa kisha unapuuzwa kimya kimya
 
FB_IMG_1617350591196.jpg
 
#Chumvi haitakufaa kwa chai asubuhi, ila itakufaa kwa mboga mchana.

Usivunje uhusiano na mtu sababu tu umegundua kuwa sio rafiki.

Kwenye maisha hatuhitaji marafiki tu. Tunahitaji watu wote.

Kila mtu atakufaa kwa namna tofauti. Hata wale wasio marafiki, kuna kipindi watakufaa.

Sio kila mtu atakufaa kwenye biashara au kipindi unatafuta kazi.

Na sio kila mtu atakufaa kipindi unajiandaa na harusi yako au kipindi unatafuta mtu wa kukukopesha.

Pia, sio kila mtu atakufaa kipindi unaumwa au kipindi umefiwa.

Jambo moja tunalokosea ni kudhani kuwa yupo mtu atakayetufaa kwa kila kitu. Na kwa namna hiyo, tumepoteza watu wengi ambao wangekua na manufaa kwetu.

Anaekufaa kwa kila kitu ni Mungu pekee. Binadamu wote watakufaa tu kwa msimu.

Kinachotakiwa ni kutambua kila mtu anaekuzunguka anakufaa kwa nini, na kumtumia kwa hicho ambacho anakufaa.

Usivunje urafiki wa miaka mitano sababu tu hakuja kwenye msiba ulipofiwa. Ndani ya miaka mitano, hakukufaa kwa jambo jingine lolote lile?

Narudia, Chumvi haitakufaa kwa chai asubuhi, ila itakufaa kwa mboga mchana

Kila mtu atakufaa katika jambo tofauti na katika nyakati tofauti. Mahusiano bora huongozwa na akili, na sio hisia.

Nawatakia kila lililo jema na Mungu awabariki
 
Back
Top Bottom