Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ajenti wa Jorginho Joao Santos amesema kiungo huyo wa kati, 29, raia wa Italia ambaye amehusishwa mara kadhaa na kurejea Napoli, sasa kuna uhakika wa "asilimia 100" kwamba atasalia Chelsea baada ya kukamilika kwa msimu huu. (Tutto Mercato - in Italian)
 
Beki wa Everton Thierry Small, 16, yuko tayari kukataa mkataba wa miaka mitatu ili atafute fursa ya kuingia katika timu ya kwanza kwengine huku Manchester United, Arsenal, Brighton na Brentford zina mnyatia. (Express)
 
Mshambuliaji wa Atalanta raia wa Colombia Duvan Zapata, 30, ambaye amehusishwa na kuhamia Chelsea na Liverpool, amesema "siku moja" atacheza katika Ligi ya Premier na kusema amekua akiwa shabiki wa Arsenal. (Gazzetta dello Sport, via Football London)
 
Na mlinzi wa Aston Villa raia wa Ubelgiji Bjorn Engels huenda akarejea katika nchi yake msimu huu huku Royal Antwerp ikimnyatia baada ya kushindwa kumsajili mnamo mwezi Januari. (VoetbalKrant, via Birmingham Mail)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…