Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

LG ni mtengenezaji mkubwa wa tatu wa simu za mkononi ulimwenguni tangu mwaka 2013 hadi miaka ya hivi karibuni na imejitahidi kutengeneza simu za mkononi katika mazingira ya ushindani mkali wa soko ambalo linajumuisha Apple, Motorola au Huawei.
 
Kuanzia mapema mwezi Januari kampuni hiyo kubwa ya elektroniki ya Korea Kusini ilisema inatafakari mbinu zote zitakazoisadia kukomesha hasara baada ya kuandikisha karibu miaka sita hasara inayokadiriwa kuwa karibu dola bilioni 4.5
 
"Uamuzi wa LG kujiondoa katika biashara ya utengenezaji simu za rununu iliyo na ushindani mkali itawezesha kampuni hiyo kuelekeza rasilimali zake katika ukuaji wa aina nyingine kama vile vifaa vya gari ya umeme, vifaa vya kuunganisha bidhaa za umeme, nyumba nzuri, roboti, akili ya bandia na kadhalika" kampuni hiyo ilisema katika taarifa yake.
 
Lakini licha ya hasara, kampuni ya ushauri ya Counterpoint inaelezea kufungwa huko ni kutokana na ukweli kwamba "wakati enzi za simu za rununu zilipoanza, LG ilipitisha mfumo wa uendeshaji wa Microsoft badala ya Android na ikachukua muda kuingia kwenye mfumo wa uendeshaji wa Google."
 
Kando na hilo lazima tuongeze kwamba LG iliamua kujiingiza katika ushindani wa kutengeza simu za rununu za hali ya juu na za wastani ambazo zinatengenezwa na kampuni zingine ambazo zilikuwa na ''ubunifu zaidi''.
 
Back
Top Bottom